EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, July 20, 2015

Penzi la Shilole na Nuh layeyuka

shilolee-3
Bongo Fleva na mwigizaji, Zuwena Mohammed a.k.a Shilole a.k.a Shishi Beiby na msanii mwenzake Nuh Mziwanda.
Na Saphyna Mlawa LILE penzi lililotikisa Bongo kati ya mwanadada mrembo ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na mwigizaji, Zuwena Mohammed a.k.a Shilole a.k.a Shishi Beiby na msanii mwenzake Nuh Mziwanda, limevunjika ghafla wikiendi iliyopita. Awali, Shishi Beiby alikuwa amekolea kimahaba kwa ‘serengeti boy’ huyo na kulikuwa na kila dalili kwamba watafunga ndoa lakini mrembo huyo ndiye aliyekuwa kwa kwanza kutangaza juzi kwamba amempiga chini Nuh.
SHILOLE390
...Wakifanya yao.
Wikiendi iliyopita, wapenzi hao waliokuwa wameshibana na kugandana kama kupe, walionyesha kwamba wameachana vibaya, baada ya kutumia mitandao ya kijamii kutukanana, kitu ambacho wengi walikiponda na kudai wanatafuta kiki kwa lazima. Championi lilipata taarifa hizo na kuamua kuwafungia kazi wote wawili na kuanza kumvutia waya Shishi Beiby ambaye alitoa ufafanuzi wa kile kinachoendelea kwenye uhusiano wao. nuhu Championi: Mambo vipi Shishi? Shishi: Mambo poa tu mzima wewe? Championi: Mi mzima aisee sijui kwa upande wako? Shishi: Niko poa pia. Championi: Vipi Ramadhani imeendaje? Shishi: Kwanza kabisa ninamshukuru Mungu kwani tumemaliza salama funga yetu, lakini pia kupitia Mfungo wa Ramadhani kuna mambo mengi ambayo nimejifunza ikiwemo, kuswali, kupenda amani, kusamehe pamoja na kuwa na hofu ya Mungu. MZIWANDA2340 Championi: Vipi imekuwaje tena mbona nasikia umeachana na kaka yetu? Shishi: Aisee ni kweli unajua Nuh ni mzinguaji, yaani licha ya kumsaidia lakini ananiletea ujinga daah! Acha afanye yake as longer as ni mwanaume na mimi ni mwanamke kila mtu atapata riziki yake mbele. Championi: Kwani tatizo ni nini, maana mlikuwa kimya wenyewe imekuwaje? Shilole: Kwa kweli mi siwezi kuzungumzia sana sababu ni mambo ya ndani kuachana naye ila we jua tu Nuh anazingua. Championi : Ok! Basi poa, nikutakie siku njema. Shilole: Asante na kwako pia. UJUMBE ALIOUTUMA SHILOLE KWENYE INSTAGRAM Shilolekiuno: Mwanaume hata umfanyie nini haridhiki lol! Pamoja na kukubali shida zake zote lakini mh! Nimejitahidi, nimehangaika ila sasa kama gari limewaka, akaaa babu weeh! Kanikuta na maisha yangu, wacha niendelee na maisha yangu, mimi na yeye baaaaaaasi #Gandalandizi. Alipotafutwa Nuhu alisema kwa kifupi: “Kuachana siyo jambo la kushangaza, kwa sababu wengi wanaachana na Mungu kapenda tuachane, kwa sasa nadili na kazi zangu tu.” MUDA MFUPI BAADAYE NUHU NAYE AKATUPA JIWE M ziwandanation: “Mwanaume wa kweli hukaa kimya, sibishani na upumbavu, mwanamke asiyeridhirika na kathaminiwa mpaka tatoo kachorwa na kuvumilia mambo yote aliyonifanyia ya kuniaibisha mbele ya mashabiki zangu, familia, wasanii wenzangu na wadau anaanza kunitukana mitandaoni for whaaat!!! mxeeeew mimi bado kijana na nina time ya kupata maisha yangu na mtu atakayethamini moyo wangu, nawaachia wanaume wenzangu na nyie mjaribu zari #Ashangedere. ALICHOSEMA SHILOLE ALIPOZUNGUMZA NA CHAMPIONI WIKI MOJA ILIYOPITA KUHUSIANA NA PENZI LAKE KWA NUH Jamani Nuh siyo mdogo ila ni mwili wake tu, lakini pia kama wanaona ni mdogo basi ni kwa upande wao na mtazamo wao, kama angekuwa mdogo mbona mimi ananiridhisha sana kwenye mambo yetu? Hakuna mfano, ndiyo maana tumetulizana.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate