EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, August 19, 2015

Dude: Usiingize sanaa kwenye ndoa yako

dude2
Kulwa Kikumba ‘Dude’.
KWAKO Kulwa Kikumba ‘Dude’. Habari za siku ndugu yangu. Kitambo kidogo hatujaonana ana kwa ana, labda kwa kuwa wote tupo bize na ndiyo maana leo nimekukumbuka kupitia barua.
Ukitaka kujua afya yangu, mimi sijambo. Hofu na shaka ni kwako wewe uliye mbali na upeo wa macho yangu. Vipi wanao wote hawajambo? Shemeji je?
Dhumuni la barua hii ni kutaka kukueleza kwamba nimeona tatizo katika maisha yako ya kawaida. Umekuwa ukiingiza maigizo kwenye ndoa yako.
Mara kadhaa umewahi kunaswa na magazeti Pendwa ukiwa katika pozi tata na msanii mwenzako, Ester Kiama.

Mara nyingi umekuwa ukikanusha kwamba hauna uhusiano wa kimapenzi na msanii huyo zaidi ya kufanya naye kazi. Mimi sikubaliani na hilo. Unauongopea umma.
Mazingira yanakuhukumu. Haiingii akilini mtu ambaye mnafanya naye kazi, kila wakati mnakuwa ‘beneti’ hata katika shughuli ambazo si za kikazi.
Mbaya zaidi nimewahi kumnukuu akidai wewe ni mtu wake wa karibu, unayehakikisha kwamba gari lina mafuta. Eti wewe ni ‘fundi’ wake, hata gari likiharibika.
Umewahi kukutwa nyumbani kwa Ester, inasemekana huwa mnapika na kupakua nyumbani kwake. Wewe ni baba wa familia. Una mke, iweje uiache familia uende kula na wakati mwingine kulala kwa msanii mwenzako? Si busara.
Kitendo tu cha wewe kwenda kupima Ukimwi na Ester kilichoripotiwa katika vyombo vya habari wiki iliyopita, kilitosha kuthibitisha mlikuwa na uhusiano gani. Sasa kwa nini uendelee kuishi katika mazingira ya aina hii?
Imefika hatua kweli hata mkeo anaamua kuondoka nyumbani kutokana na wewe kukolea kwa Ester? Unataka kuifanya jamii iamini kwamba maisha ya wasanii ndivyo yalivyo. Kwamba yale mnayotuonesha katika sinema, kubadilisha wanawake ndiyo maisha yenu?
Nakushauri ndugu yangu, kutokana na muda mrefu ulioishi na mkeo, huna sababu ya kuishi ‘kihunihuni’. Tulia na mama. Una familia yenye watoto saba, walee wanao. Maisha ya kimjinimjini hufanani nayo.
Wanao wanakutazama. Wewe ndiyo dira. Ukionesha njia mbaya, watajifunza nini kutoka kwako? Nakuamini, kwa kuwa shemeji amesharidhia kurudi nyumbani, onesha mapenzi.
Dumisha penzi lako na mfurahie maisha yenu kama ilivyokuwa hapo awali.
Ni matumaini yangu utakuwa umenielewa. Fanyia kazi hayo yote na kamwe usikubali sanaa unayoifanya kwenye video iingie katika maisha yako ya kawaida.
Ni mimi nduguyo,
..................
Erick Evarist

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate