EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Monday, August 17, 2015

Jokate amtambulisha Ali Kiba apigwa chini kwao

jokate ali kiba
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ akiwa na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
Musa mateja Imevuja! Gumzo la ndoa ya staa mwenye jina kubwa Bongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ inadaiwa kupigwa zengwe kama ilivyowahi kutokea kwa Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kufuatia madai ya mwanadada huyo kumtambulisha jamaa huyo kwao kisha kukataliwa. MINONG’ONO Habari kutoka chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa wawili hao, tukio hilo lilijiri hivi karibuni ambapo wawili hao walihudhuria kwenye harusi ya dada wa Jokate hivyo kuibua minong’ono kwamba huenda harusi inayofuata itakuwa yao. Chanzo hicho kiliendelea kudai kwamba, habari mbaya ni kuwa baada ya Jokate kumtambulisha Kiba kwa ndugu, jamaa na marafiki baadaye kumpeleka kwao, wazazi wa mwanadada huyo walikuja juu wakidai jambo hilo haliwezekani huku sababu nne zikianikwa. jokate
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
KIGEZO CHA DINI Madai yalishushwa kuwa, sababu ya kwanza ni kwamba, familia ya Jokate hasa wazazi wake ni watu walioshika sana Dini ya Kikristo (Kanisa Katoliki) huku Kiba akiwa ni Muislam kama ilivyokuwa kwa Diamond aliyeshindwa kumuoa Jokate kwa kigezo hichohicho. NDOA ZA MASTAA NI TATIZO? Ilidaiwa kuwa, sababu ya pili iliyotolewa na wazazi hao ni kwamba, hawataki binti yao kuolewa na msanii mwenzake kwa kuwa wanajua ndoa za mastaa zinavyokuwa na ‘drama’. KIGEZO CHA KABILA Kigezo kingine kilichotajwa ni kabila ambapo wazazi hao wanataka Jokate aolewe na mtu wa kabila lake la Wangoni tofauti na Kiba ambaye ni Muha. 2alikiba-1
Mbongo-Fleva Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’.
KIGEZO CHA BONGO FLEVA Chanzo kilikwenda mbali zaidi na kudai kuwa, wazazi hao wanaamini kwamba baadhi ya wasanii wa Bongo Fleva ni wahuni hivyo kuwawia vigumu kukubali binti yao kuolewa na Mbongo-Fleva.Pia habari za ndani zilidai kwamba, Jokate na Kiba walikuwa kwenye harakati za kuoana kabla ya mwaka huu kumalizika ila zengwe limekuwa kubwa upande wa familia hasa kwenye suala la dini ambapo kila mmoja amekuwa akitaka mwanaye abadili dini. KAMA DIAMOND “Unajua kilichompata Kiba ni kama kile kilichomfika Diamond kipindi kile alipotaka kumuoa Jokate. “Ilikuwa ni ishu hiyohiyo ya dini maana wazazi wa Jokate walikuwa wakimwambia kila siku kama kweli anampenda mtoto wao basi abadili dini lakini Diamond hakuweza kufanya hivyo na kujikuta wakishindwa kufikia lengo la kufunga ndoa,” kilitambaa chanzo hicho. KIBA KAMA KAWA Kama kawaida yake, Kiba alipoulizwa juu ya ishu hiyo alikanusha vikali akidai kwamba hajawahi kuwa na mipango hiyo na mrembo huyo.“Ulishawahi kunisikia nikizungumzia ishu hiyo? Siyo kweli bwana…hakuna kitu kama hicho,” alisema Kiba akionekana ‘kumaindi’ kwa kuulizwa juu ya jambo hilo.Kwa upande wake Jokate hakupatikana hewani na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu hivyo jitihada za kumpata zinaendelea. TUJIKUMBUSHE Kwa muda mrefu, Jokate na Kiba wamekuwa wakiripotiwa kuwa ni wapenzi lakini Kiba amekuwa mstari wa mbele kukanusha huku Jokate akikiri kuwa jamaa huyo ni mtu wake.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ Redd’s Miss IFM REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate