EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, August 28, 2013

CHOMBEZO:KITANDA CHA MAMA MWENYE NYUMBA....SEHEMU YA ...05

Na Irene Mwamfupe Ndauka
  ILIPOISHIA:
“Mungu wangu…atakuwa nani huyo..?”
Fuko alivaa nguo zake na kufungua mlango ili
atoke mbio, akakutana na macho ya mfanyakazi wa ndani…
“Ha!” alihamaki mfanyakazi…
“Ooosh,” mlinzi naye alishutuka akarudi
chumbani…
 
“Sasa wewe unatokaje bila kuniambia, je
ukikutana na huyo mama wa kazi itakuwaje?” alihoji mama Joy…
“Siyo nikikutana naye, nimekutana naye kweli,
amesimama hapo mlangoni…”
“Kweli..?”
“Kweli bosi.”
Yule mfanyakazi alipokutana na macho ya
mlinzi, alitoka mbio kwenda jikoni huku mapigo ya moyo yakimwenda kwa kasi ya
ajabu…
 
“Oo…ooo…”alihema…
“Ina…ina maana…ina maana mama na Fuko ni
wapenzi? Hivi ina…inawezekana kweli..?”
Mama Joy alifungua mlango, hakukuta
mfanyakazi wale msaidizi wake, akatembea kuelekea jikoni, akasikia mlio wa
mfuniko kwenye sufuria, akarudi chumbani mbio…
“Toka sasa, yupo jikoni…”
“Hawezi kuniona..?”
“Nimekwambia yuko jikoni sasa atakuonaje?”
 
Mlinzi alitoka mbio. Kufika nje akasikia
geti kubwa linagongwa, akaweweseka kwanza kabla ya kwenda kumjua anayegonga…
“Siyo bosi huyo…kama ni yeye amerudi saa
ngapi? Hajatuona kweli..?”
Alikimbilia getini, alipogundua bado
kulikuwa na kufuli, aliingia kwenda banda na kuchukua funguo…
“Ngo ngo ngooo…”
“Nani?”
“Mimi…”
“Wewe nani..?”

“Mzoa taka…”

“Unataka nini, leo hakuna takataka hapa
ndani, halafu…”
“Mama je..?”
“Mama gani, we mama yako anaishi humu ndani
kwani..?”
“Mama mwenye nyumba…”
“Kwani kama hakuna taka, mama wa nini sasa?”
“Sikiliza bro, mi sioni ni kwanini
unanichukia, wewe unapata liziki yako kivyako na mimi napata kivyangu, sasa…”
 
“Fuko ni nani huyo?” mama Joy alihoji akiwa
amesimama mlango mkubwa macho kayaelekeza getini…
“Mzoa taka mama, simi sijui anataka nini
mama, kwani leo kuna takataka humu ndani, mimi sijaziona,” alisema sana mlinzi…
“Wewe hujaziona kwani we ndiyo mzalisha
taka? Hebu mfungulie.”
 
Mlinzi alifungua geti haraka sana, mzoa taka
akaingia huku akiwa amebeba fuko la Rambo mgongoni…
“Karibu kijana wangu…”
“Asante mama, shikamoo…”
“Asante sana. Karibu pita.”
Mzoa taka alizama ndani ya geti akimfuata
mama. Nyuma yake, mlinzi alikuwa akimwangalia kwa jicho baya ile mbaya…
“Mama mi nina wazo,” alisema mlinzi…
“Liweke wazi…”
 
“Hilo dude la taka lingejengwa nje…”
“Si jukumu lako,” alijibu mama Joy.
Mlinzi aliumia sana moyoni. Aliamini mzoa
taka ana jambo na bosi wake, haiwezekani usiku kucha ampe mapenzi motomoto tena
kitandani kwa mumewe, kisha asubuhi hiyo aanze kumgeuzia kibao na kuongea naye
kama vile siku nyingine za nyuma. Alimezea lakini akaweka kitu moyoni.
 
Mama Joy alimshika mkono mzoa taka na kwenda
naye nyuma ya nyumba ambako kuna dude la taka…
“Hivi kijana wangu unaitwa nani vile..?”
“Kofu…”
“Kofu..?”
“Ndiyo…”
 
“Kofu nani?”
“Kofu Nduche…”
“Mbona jina lako limefanana sana na la
mlinzi wangu yule..?”
“Yeye anaitwa nani?”
“Fuko…”
 
“Sasa mama Fuko ni sawa na Kofu..?”
“Eee, Fuko ukiigeuza na kuanzia kwa mbele si
unapata Kofu…”
“Eee, kweli. Basi ndiyo hivyo.”
Walipofika kwenye dude la taka, mzoa taka
alichungulia ndani ya dude na kukutana na taka kidogo sana…
“Leo hamna kitu mama…”
 
“Wewe shida yako nini, si nakupa hela yako
ya kuzolea…au?”
“Sawa,” alisema mzoa taka huku akianza
kuingiza sehemu ya mwili kwenye dude hilo kwa lengo la kuchota takataka kidogo
zilizokuwepo.
 
Mama Joy alimsogelea Kofu na kumshika kiuno
kisha akamvuta. Jamaa alichomoka, akasimama akimwangalia mwanamke huyo…
“Vipi, leo hutaki?” aliuliza mama Joy huku
akiwa amelegea macho kama aliyekula kungu manga…
“Sijui wewe…”
 
“Mimi niko tayari,” alisema mama Joy…
“Hata mimi, lakini leo nimechoka sana…”
“Umechokeshwa na nini?”
“Sijatia kitu tumboni tangu nimeamka.”
“Hilo tu, twende huku,” mama Joy alimshika
mkono mzoa taka na kwenda naye hadi jikoni kwake…
“Kuna nini?”
 
Mfanyakazi wa ndani akafunua sufuria moja…
“Kuna hili pilau, halafu kuna nyama
imeshaiva, ila kwenye friji kuna mikate na maandazi, keki zipo mezani, chapati
zipo kwenye hotpot, lakini kama utataka samaki wa kukaanga wapo tayari kwenye
friji ni wa kupasha moto tu…”
 
“Mh! Mwenzetu umetaja vitu vingi hadi
nimesahau vya kwanza…mpe huyu maziwa na pilau,” alisema mama Joy. Alijua kwa
kazi ya kuzoa taka mchana kutwa na kama toka ameamka hajatia kitu tumboni,
alitakiwa chakula kizito kidogo…
 
“Kaa pale kwenye kiti.”
Mzoa taka alikaa akisubiri kifungua kinywa
hicho ambapo moyoni alisema atakula mpaka kukomba sahani na akitoka pale ni
mpaka kesho yake, fedha yote ya siku hiyo atakwenda kununulia bangi na kupiga
viroba kwa wingi.
 
Mama Joy alikwenda chumbani kwake, akabadili
nguo. Alivaa taulo akaingia bafuni kuoga. Alipotoka, alivaa khanga mbili, moja
alijizungusha kupitia kwenye nido zake, nyingine kupitia kiunoni. 
Akatoka kwenda jikoni ambako alimkuta mzoa
taka yuko katikati ya mlo wa pilau na maziwa kwenye kikombe kikubwa…
“Vipi, changamka upate nguvu…”
“Sawa mama…”
 
Mama Joy naye alichukua kikombe na
kujimiminia maziwa peke yake…
“Nikupe na nini mama?” aliuliza mfanyakazi…
“Hapana, maziwa yanatosha sana.”
Ukimya ulitawala jikoni, mzoa taka alikuwa
akiendelea kupata ‘brekfasti’ yake, mama Joy alikuwa bize na maziwa yake huku
mfanyakazi naye akijihudumia mwenyewe.
Mzoa taka alitangulia kumaliza kila kitu…
 
“Hebu muongeze mgeni maziwa na pilau,”
alisema mama Joy lakini mzoa taka aligoma. Ilikuwa lazima agome hata kama
anavuta bangi. Maana wavuta bangi wanasifika kwa kula sana, lakini pale alipewa
maziwa kwenye kombe kubwa, pilau kwenye sinia na si sahani…
“Mimi nimeshiba sana…”
 
“Ongeza japo kidogo, we mwanaume bwana,”
alisema mama Joy…
“Hapana mama, kesho.”
Mama Joy naye alitelekeza kikombe chake
chenye maziwa na kutoka na mzoa taka hadi kwenye dude la taka…
“Sasa, si tayari umeshiba?”
 
“Nimeshiba sasa…teh! Teh! Teh!” alicheka
mzoa taka huyo huku jasho jembamba la shibe likimchuruzika kuanzia kichwani.
Mama Joy alimsogelea mpaka akamkumbatia,
akampiga busu. Mzoa taka naye akamrudishia kwa busu. Mama Joy akaenda mbele
zaidi, akaomba denda licha ya kwamba kinywa cha mzoa taka huyo kilikuwa kikitoa
harufu ya sigara.
 
“Mwee, ulimi wako una kajoto kazuri,”
alisema mama Joy huku akimung’unya mate ya mzoa taka huyo ambaye mwenyewe
alikuwa akijiuliza ni kwanini mwanamke huyo mwenye mume tajiri ameangukia kwake
tena mchafumchafu asiye na thamani mbele za watu.
 
Aliwaza jinsi wanawake mitaani wanavyomkataa
kwa sababu ya uchafu wake na mibangi anayovuta…
“Mm…au mganga wake alimwambia atembee na
mwanaume mchafumchacfu nini?” alijihoji mwenyewe. 
 
Mama Joy, licha ya kulala na kuamka na
mlinzi wake, lakini muda huo alijikuta akichemka kwa kutaka penzi tena.
Alimshika mzoa taka na kumlaza pembeni ya
dude la taka, akamvua nguo, akavua na zake, wakaanza ligi ya mapenzi huku
mwanamke huyo akimiminika wingi wa maneno ya mahaba.
 
Mlinzi, yaani Fuko alihisi kuna kitu
kinachoendelea kwenye dude la taka kwa vile toka bosi wake huyo alivyomshika
mkono mzoa taka na kuzama naye maeneo hayo hakurejea tena, hakujua kama mzoa
taka alipelekwa hadi jikoni akala pilau na maziwa.
 
Alisukuma geti kulifunga lote kisha akaanza
kutembea kuelekea kwenye dude la taka, aliamini atakutana na fumanizi japo
akili nyingine ilimwambia endapo atawafumani kweli ajue na kibarua kitakuwa
kimeota nyasi.
 
Upande mwingine alijua hawezi kufukuwa kwa
sababu ishu si kikazi ila wivu wa kimapenzi…
“Itakuwa alale na mimi halafu mzoa taka kaja
anampapatikia vile, lazima kuna kitu wanakifanya,” alisema moyoni mlinzi.
 
Alipotokea kwa mbali alianza kuona miguu
minne ikiwa imefungana pamoja, akashtuka…
“Si nilisema mimi,” alisema moyoni. Miguu
hiyo ilikuwa ikipishanapishana kwa kuingiliana kwa staili mbalimbali. Mlinzi
aliweza hata kujua miguu ya mzoa taka ni ipi na ya tajiri yake ni ipi.
Alichofanya, alikimbilia jikoni kwa
mfanyakazi wa ndani…
 
“Dada nanihii, nenda kwenye dude la taka
haraka sana ukaone…”
“Kuna nini kwani Fuko..?”
“Nimekwambia we nenda, husikii…”
“Sasa nitakimbilia sehemu kutazama kitu
ambacho sikijui, pengine nikikiona nitaogopa je?”
“Shauri zako,” alisema mlinzi na kutoka.
 
Nyuma, mfanyakazi huyo aliamua kwenda kwenye
dude la taka huku akili yake ikiwa haiwazi atakutana na kitu gani.
“Ha..!” alishtuka sana mfanyakazi huyo
ambaye kiumri alikuwa amempita mama Joy.
Mama Joy naye alishtuka kusikia hamaki ya
mfanyakazi wake, akamsukuma mzoa taka kisha yeye akasimama haraka sana huku
akihema kwa kasi…
 
“Mama…” alisema yule mfanyakazi…
“Mama nini? Unasemaje kwanza?”
Mfanyakazi alikimbilia ndani huku akilia.
Kwake yeye kitendo alichokiona alikichukulia kama nuksi au mkosi, pia alihisi
kujidhalilisha nafsi kwani hakukitegemea..
“Yaani bosi! Anazini na mtoto mdogo yule!
Tena mchafuuu! Mh! Ama kweli dunia imekwisha! Loo!” mfanyakazi huyo alisema
hayo moyoni mwake.

***

Mama Joy, baada ya kumwona mfanyakazi wake
amekimbia, alihisi heshima kubwa amepata…
“Mimi naona twende chumbani kwangu, hapa
wala siko huru, kama ameanza kuja huyu anaweza kutokea mwingine,” mama Joy
alimwambia mzoa taka…
“Chumbani mwako! Kitandani?” mzoa taka
alishangaa na kumuuliza…
“Kwani kuna nini?”
 
Wakati mama Joy anamwambia mzoa taka kwani
kuna nini, alishamshika mkono na kwenda naye kupita kwenye mlango mdogo wa
nyuma ambapo si rahisi kuonwa na mtu.
Mlinzi pale getini alikwenda tena kwa
kunyata hadi akafika eneo ambalo kuna nguzo nene, akasimama ili ajipange tena
kwenda jirani na dude la taka…
 
“Safari hii nikiwakuta bado wanazini
nawafumania, nitamwambia bosi habari hii nitamwambia mume wake akirudi safari,
najua hatataka,” alisema moyoni mlinzi.
Alishangaa sana kutowakuta pale chiji ya
dude la taka, akabaki kutumbua macho pima huku akijiuliza ni wapi wawili hao
wanaweza kuwa wamekwenda kumalizia kula ‘uraha’ wao…
 
“Au wamekwenda choo cha nje kule?
Haiwezekani! Labda wamekwenda kule nyuma kabisa,” alisema huku akienda nyuma ya
nyumba ambako pia hakuwakuta…
“He! Au wameingia ndani kabisa?”
Alikwenda jikoni, akamkuta yule mwanamke wa
kazi amekaa kwenye kiti huku akilia…
“Nini tena? Amekufokea?”
 
“Mh! Siwezi kulia kwa kufokewa na tajiri
wangu wa kazi hata siku moja, ila mimi nimemshangaa sana bosi, yule kijana ni
mchafu sana halafu sijui anavuta bangi. Lakini eti yeye amelala naye kama
mpenzi wake! Unajua sijawahi kusikia achilia mbali kuona,” alilalama mwanamke
wa kazi…
“Kwani uliwakutaje?” mlinzi aliuliza…
“Wako ‘kazini’…”
“Walipokuona?”
 
“Mama akamsukuma yule kijana, halafu akaanza
kunijia juu, mimi nikaondoka,” alisema mfanyakazi wa ndani huku
akiangaliaangalia nje kwa tahadhari kubwa…
“Mama huyu…”
“Lakini we Fuko, mbona na wewe umelala kwa bosi usiku wa kuamkia leo?”
“Si ndiyo hapo sasa hata mi mwenyewe
najiuliza, kwanini alale na mimi halafu alale na mzoa taka? Usikute ni mambo ya
kishirikina,” alisema mlinzi…
 
“Kwani wewe ulikuwaje hadi mkalala kitandani
na kuzini?”
“Alinitongoza..!”
“Alikutongoza..?”
“Sasa wewe dada unavyoona mimi naweza
kumtongoza huyu bosi, nitaanzia wapi kwanza? Au unadhani mzoa taka alimtongoza?
Huyu mama ni mtaalam wa kutongoza, huenda hata mumewe alimtongoza.”

***
Mama Joy alimtumbukiza chumbani kwake mzoa
taka ambaye alifikia kushangaashangaa chumba kilivyo kikubwa na vitu vingi…
“Mh! Si nitachafua hapa leo?” ndani ya moyo
wake aliamini hivyo…
Alimshika kijana huyo na kumuegemeza kifuani
kwake huku akimwambia maneno matamu ya mahaba…
 
“Mpenzi wangu, nataka nikiachana na wewe leo
nisitamani mwanamke mwingine mpaka ipite wiki moja, sawa?”
“Sijakulewa.”
“Nasema hivi, tukipanda kitandani sasa hivi
ufanye mambo mazuri sana, nataka tukimaliza leo nisiwe na hamu ya mwanaume
mpaka wiki moja ipite.”
“Sawa.”
 
Mama Joy alimvua nguo mzoa taka na kubaki na
‘kufuli’ tu, kisha akavua na za kwake. Alitangulia kupanda kitandani, mzoa taka
akafuatia akiwa na wasiwasi, hamu ya mapenzi hakuwa nayo kama ilivyokuwa kule
nje kwani mazingira ya chumba na alivyo yeye vilikuwa vitu viwili tofauti…
 
“Sijui ananisema mi mchafu sana,” aliwaza…
“Sasa mbona jogoo mwenyewe hawiki, una
nini?” aliuliza mama Joy huku akijaribu ‘kumtoa’ jogoo kwenye banda ili aende
nje akawike, lakini wapi! 
“Kijana, una nini mpenzi wangu, mbona
hivi..?”
 
“Hata mi sijui, lakini tungeenda kule nje
kwenye majani ndiyo kuzuri…”
“Mimi nje siwezi, we si umeona hali
ilivyokuwa kule nje, kwani tatizo lako nini?”
“Sina uhuru na humu chumbani kwako, kuko
kama ikulu bwana…”
“Umewahi kufika ikulu wewe?”
 
“Si wanasemaga kuzuri sana…”
“Sasa ikulu hakuna wafanyakazi wa kufanya
usafi?”
“Mi sijui, lakini bado naogopa sana…”
“Unamuogopa mume wangu..?”
“Hapana, ila ntachafua…”
“Nini..?”
 
“Mashuka yako, mi sijaoga toka juzi ilee.”
“Wala usijali, mfanyakazi yupo atafua
mashuka, we tulale hapahapa, lakini fanya nilivyokwambia, nikomeshe kabisa
leo,” alisema mama Joy huku akipeleka mkono kwenye jogoo la mzoa taka huyo.
Kwa mbali, alianza kuwika kwani mzoa taka
alihakikishiwa amani yake.

***
Fuko na mfanyakazi wa ndani walitoka kiaina
kwenda kuwachungulia wawili hao kule nje, wakawakosa…
“Ha! Watakuwa wamekwenda wapi?” aliuliza
mlinzi…
“Hawa wamekwenda chumbani. Hakuna sehemu
nyingine wanayoweza kwenda zaidi ya huko,” alijibu mfanyakazi.


***
Baba Joy alikuwa amemaliza mambo
yaliyompeleka Arusha, sasa alikuwa amekaa kwenye mgahawa akibadilishana mawazo
na wenyeji wake…
“Unajua bwana, mwanamke siku zote anatakiwa
kujitambua. Ukikuta mwanamke hajitambui ujue kazi unayo we mwanaume…” alisema
mmoja wa wenyeji hao aitwaye Molleli…
“Ni kweli. Wanawake wa sasa wengi hawajijui.
Utakuta mwanamke mke wa mtu lakini bado anapenda magenge, anapenda makundi,
anataka awe anatoka na marafiki zake. Halafu ogopa sana mke wa mtu akiwa
anapenda kuwa na ukaribu na vijana vijana…”
 
Baba Joy aliguna hapo. Akakumbuka jinsi
mkewe alivyo na ukaribu na mzoa taka kiasi cha kumkaribisha ndani kwake hata
giza likiwa limeingia.
Palepale alichukua simu yake iliyokuwa
mezani na kumpigia simu mlinzi…
“Hujambo Fuko..?”
“Sijambo bosi, shikamoo…”
“Marhaba, mama Joy yupo..?”
“Yupo bosi…”
“Na nani..?”
 
“Unasema..?”
“Nakuuliza yupo na nani..?”
“Nani mama..?”
“We una akili kweli? Unadhani nakuuliza
kuhusu nani..?”
“Nimekujibu bosi, nimesema mama yupo…”
“Yupo na nani..?”
“Unasema?”
Baba Joy alikata simu kwa hasira. Lakini
akili ikamwambia kuna kitu ndiyo maana mlinzi anajibu maswali yote kasoro hilo
tu! Aliisachi namba ya mkewe, akampigia.

***
Mama Joy alikuwa akimbembeleza mzoa taka
akubali kulala kitandani na aondoe mawazo kwani ndiyo yanayomfanya jogoo
ashindwe kuwika….
“Haa! Mume wangu huyo anapiga…
“Haloo…”
 
“Uko wapi wewe..?”
“Nani mimi..?”
“Unaniuiliza swali gani hilo..?”
“Niko nyumbani…”
“Na nani..?”
“Nani mimi..?”
“Mama Joy…”
“Abee…”
Baba Joy alikata simu. Alianza kuhisi kitu
kikubwa zaidi. Akampigia mfanyakazi wa ndani…
“Za safari bosi..?”
“Njema, upo nyumbani..?”
“Ndiyo bosi…”
“Mama je..?”
 
Na muandishi wako IRENE MWAMFUPE NDAUKA Usikose sehemu ya 06 siki ya Jumamosi ya wiki hii hapa....

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate