Kuna ajali imetokea usiku huu Kibaha Maili Moja ambapo lori 'semi trela'
limeanguka na kufunga barabara hivyo kusababisha foleni kubwa kwa
magari yanayokwenda Dar na mikoani.
Kwa mujibu wa shuhuda, ajali hiyo imetokea majira ya saa mbili usiku ambapo lori hilo lilikuwa likitokea mkoani kwenda Dar, lilipopita mizani lilianguka na kufunga barabara kona moja hadi nyingine.
Abiria waliokuwa kwemye mabasi kutoka mikoani, wamelazimika kulala ndani ya mabasi, wengine walishuka na kupanda bodaboda kwenda au kutembea kwa miguu kwenda upande wa pili.
Mabasi yaliyoathirika na kadhia hiyo ni pamoja na Zubeir, Mohamed Trans, Sai Baba, Najimunisa na mengine kibao.
Habari zinasema, jitihada zilikuwa zikifanyika kupeleka breakdown kutoka mamlaka ya bandari ili kulinyanyua lori hilo na magari yaanze kupita.

No comments:
Post a Comment