Msanii
wa miziki ya kizazi kipya maarufu kama Ally Kiba akitoa burudani ya
aina yake wakati wa hafla maalum kwa wanachama wa Club E ijulikanayo
kama Club E Hollywood Glam Night iliyofanyika jijini Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki na kuhudhuriwa na mamia ya watu.Wasanii hao kwa pamoja walikuwa kivutio kikubwa kwa watu wote waliohudhuria hafla hiyo ambayo ilitengenezewa mandhari kama ya Hollywood ya Marekani kutokana na ukumbi huo kupambwa na picha mbalimbali za wacheza filamu maarufu Duniani.
Msanii wa kwanza kupanda jukwaani katika hafla hiyo alikuwa Lady Jay D ambaye aliimba nyimbo saba mfululizo akiwa na bendi yake ya Machozi kabla ya kumpisha Ally Kiba.
Wakati Ally Kiba akiwa jukwaani, Lady Jay D pia alipanda tena na kufanya onyesho la pamoja kwa kuimba wimbo wa ‘Single Boy, Single Girl’ ambao ulisababisha watu wote ukumbini humo kushangilia kwa kupiga makelele kutokana na jinsi wasanii hao walivyoweza kutumia vizuri vipaji vyao.
Mbali na wasanii hao, pia mwanamuziki anayefanya vizuri hivi sasa, Diamond Platinum hakuwaangusha mashabiki wake baada ya kuwasha moto kwa kuimba na kucheza jukwaani huku akisindikizwa na wacheza shoo wake.
Katika hatua nyinge hafla hiyo ilijumisha pia michezo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sehemu za kupiga picha na mavazi kama yanayovaliwa Hollywood, gurudumu la bahati yaani (wheel of fortune) huku wageni waalikwa wa hafla hiyo wakipata nafasi ya kushinda zawadi mbalimbali.
Club E, iliyoanzishwa mwaka 2007 huendesha shughuli mbalimbali za burudani hapa nchini hususani kwa wanachama wake na wageni waalikwa kila mwaka.
No comments:
Post a Comment