MWANAMKE mmoja, Mwanaharusi Juma (34) mkazi wa Kijiji cha
Ndulungu Wilaya ya Iramba mkoani Singida, amekimbiwa na mumewe kutokana na
kujifungua watoto wawili wanaofanana na nyani.
Mama huyo mwenye familia ya watoto wanne wenye baba wawili tofauti,
aliolewa na mume wa kwanza na kuzaa naye mtoto mmoja, Fadhila Juma (15)
mwaka 2007 - mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi
Ndulungu, kabla ya kuolewa na Sadick Selemani ambaye amemkimbia baada ya
kumzalia watoto hao wawili wenye kasoro kimaumbile.
“Niliolewa na Sadick mwaka 2008 na nimeishi naye kwa miaka kumi
nikampatia watoto watatu, wakiwemo wawili wanaofanana na nyani, na mmoja
alikuwa kawaida kama binadamu wengine,” alisema.
Alisema kuwa watoto hao licha ya kuwa binadamu, lakini wamekuwa na sura za wanyama.
Mama huyo aliwataja watoto watatu aliozaa na Sadick kuwa ni Alhaji
Sadick (10), Ramadhani Sadick (6) wa darasa la kwanza katika Shule ya
Msingi Ndulungu na Abdulatifu Sadick (5).
Alibainisha kuwa, watoto hao wenye matatizo wamekuwa wakishindwa
kutembea mwendo mrefu bila kupumzika na kupumua kwa shida sana na
matumbo yao ni makubwa.
“Matumbo ya watoto wangu wawili wenye matatizo ni makubwa, macho yao
ni mekundu kama mnavyoyaona, na hupumua kwa shida sana kiasi cha
kuwafanya washindwe kutembea umbali mrefu bila kupumzika,” alisisitiza
Mwanaharusi.
Alisema kuwa, watoto hao walizaliwa wakiwa katika hali ya kawaida
kabisa, lakini walianza kuugua mara kwa mara na kutoongea tena hadi hivi
sasa.
“Mimi ni mke mdogo katika ndoa ya wake wawili, na mume wangu alipoona
nimeanza kumbana sana kuhusu matibabu ya watoto hao, aliondoka mwaka
2010 na kuhamia kwa mke mkubwa,” alisema.
Habari na Jumbe Ismailly, Singida wa Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment