Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson
Thobias a.k.a Kush aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy,
amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao Kipawa. Aligongwa akiwa
anasikiliza muziki kwa headphones huku akichati katika simu yake wakati
akitembea kwenye reli.
Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.
Marehemu Jackson ndiye aliyeshinda
kwenye Tokelezeiyer Inter-School Concert iliyoandaliwa na kundi la
Friends 4 Friends tarehe 12 Mei 2012, pia alishinda Dougie Competition
wakati 5Select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.
Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na
ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya
marehemu Jackson Thobias kwa amani, Amen.
PICHA/HABARI NA www.mohammeddewji.com/blog
Jackson Thobias a.k.a Kush enzi za uhai wake.
No comments:
Post a Comment