Ishu ambayo imewashangaza wengi
ni pale ambapo mwakilishi wa Kenya kwenye jumba la Big Brother CMB
Prezzo kutangaza kwamba amechoka maisha ya kuishi kama mfungwa kwenye
jumba hilo.
Mtandao wa Ghafla Kenya
umeripoti kwamba hii ishu imetokea wakati Big Brother alipotangaza
kupiga marufuku pombe kwa washiriki ndani ya jumba hilo, Prezzo
alishikwa hasira na kusema kwamba anaweza kuondoka muda wowote, na
anahisi wakati umefika.
Prezzo alimaind mpaka akawa
anabishana na washiriki wenzake akiwemo Keita na kutaka mlango
ufunguliwe aondoke lakini baadhi ya washiriki wenzake walimsihi asifanye
hivyo.
Huu mchongo umetokea siku 30
baada ya Prezzo kuwa trending topic kwa wakenya kutokana na kuchaguliwa
kwake kwenda big brother ambapo wengi walikua wanamdiss kwamba
haikutakiwa apelekwe BBA ambapo Nakumbuka Naziz wa Necessary Noise ambae
ni mshkaji wa Prezzo alikaa na mimi studio siku 31 zilizopita na
kuamplfy kwamba wengi wamemkosoa lakini ni kwa sababu hawamjui Prezzo

No comments:
Post a Comment