MASHABIKI na wanachama wa Klabu ya Simba wametofautiana juu ya
kuondoka kwa beki wao Kelvin Yondani, wengine wakisema ni pigo na
wengine, hapana.
Wakizunguzmia jambo hilo, baadhi yao wameweka wazi, Yondani alikuwa
mchezaji muhimu kwenye kikosi hicho, lakini wengine wakisema kwa muda
mrefu alikuwa akiipenda Yanga.
Baadhi ya mashabiki wamemtakia mafanikio huko kwa watani zao Yanga, kwani amekwenda kutafuta maisha.
Hata hivyo, wengine walitoa lawama kwa Yanga kumsajili Yondani licha ya kuwa na mkataba wa kuichezea Simba.
“Hata hivyo, Mwenyekiti (Ismail Aden Rage), yaonekana ana matatizo ya
kiuongozi, amekuwa mtu wa maneno sana bila vitendo,” alisema shabiki
Salum Ally.
Salum alisema, inasikitisha kuona Rage akiwaondoa hofu wanachama na
wapenzi wa Simba kuwa Yondani hatakwenda Yanga, lakini ameanza mazoezi.
Alisema uzembe wa viongozi wa Simba, ndio umekuwa ukikwamisha mambo
kwani Yondani, alikuwa bado mchezaji muhimu katika safu ya ulinzi ya
Simba.
Hata hivyo, shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Ally Mohamed,
alisema ingawa inauma kuona Yondani akiondoka, lakini hakuna budi kusaka
mrithi wake.
Kwa upande wake Immanuel John, alisema haamini kama Yondani amekwenda Yanga, akitaka juhudi zifanywe kubaini uhalali wake.

No comments:
Post a Comment