EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, June 24, 2012

Madaktari wagoma

Wakaidi amri ya mahakama, wasema watafia jela.
HATIMAYE madaktari nchini jana walianza mgomo usio na kikomo kwa lengo la kuishinikiza serikali kuwatimizia matihaji yao ikiwamo kuboresha mazingira ya kufanyia kazi pamoja na kuwapandishia mishahara.

Uamuzi huo wa madaktari unapingana na amri ya Mahakama Kuu Tanzania, Kitengo cha Kazi ambayo juzi ilizuia mgomo huo baada ya kupokea maombi namba 73 ya 2012 yaliyowasilishwa chini ya hati ya dharura na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Chama cha Madaktari Tanzania (MAT).
Mahakama hiyo ilitoa amri ya kusitisha mgomo huo mpaka hapo shauri la pande zote mbili (Serikali na Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama hiyo iliyotolewa juzi jioni na kusambazwa kwenye vyombo vya habari, imewataka MAT na wanachama wake kutoshiriki kwenye mgomo huo.

Mgomo waanza
Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili iliyopo jijini Dar es Salaam huduma za dharura zinatarajiwa kusitishwa wakati wowote kuanzia sasa.
Mgomo huo unaanza wiki mbili baada ya madaktari hao kuitaka serikali itekeleze madai yao la sivyo jana wangeanza mgomo usio na kikomo.
Tanzania Daima Jumapili, lilitembelea hospitali za Jiji la Dar es Salaam ikiwemo Muhimbili na zile za mkoa ambazo ni Temeke, Amana na Mwananyamala na kushuhudia kusuasua kwa huduma.
Vitengo vya dharura katika hospitali hizo viliendelea kupokea wagonjwa huku baadhi ya madaktari wakiweka wazi kuwa kuna uwezekano wa huduma hizo kusimama katika muda wa saa 24 kuanzia jana.

Muhimbili
Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wagonjwa walilamikia huduma zilizokuwa zikitolewa huku wengine wakisema wametelekezwa na wauguzi waliokuwa zamu.
Eneo la mapokezi baadhi ya askari walionekana wakiwaeleza wagonjwa waliofika kuwa huduma zimesimama na kuwasihi waondoke eneo hilo.
Mgonjwa mmoja ambaye alionekana kuchanganyikiwa alisikika akisema kuwa alimkabidhi nchi Rais Jakaya Kikwete lakini haieleweki kiongozi huyo anakoipeleka.
“Rais Kikwete nilikukabidhi nchi hii sasa unaipeleka wapi?” alisikika akisema.
John Kobelo, alisema kuwa tangu juzi kijana wake alitakiwa kufanyiwa upasuaji lakini ilipofika jana aliambiwa ampatie mgonjwa wake chakula kutokana na huduma hiyo kutokuwepo.

“Kwa kweli hali inasikitisha na kukatisha tamaa, sijui nchi hii tunaelekea wapi maana viongozi wanaamua kwa makusudi kuchezea uhai wa Watanzania,” alisikika baba mmoja akilalamika.
Tanzania Daima Jumapili ilifika katika wodi ya Sewa Haji na kukutana na mgonjwa ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake lakini alilalamikia kitendo cha madaktari kushindwa kupita zamu kwa siku ya jana huku huduma zikiwa zimezorota.
Katika wodi ya Kibasila gazeti hili lilikutana na baadhi ya wanajeshi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao walikuwa wakiangaika kumhamisha mgonjwa wao aliyekuwa akilalamika kwa maumivu makali.

Gazeti hili halikuishia hapo kwani lililazimika kufika katika Kitengo cha Mifupa (Moi) ambapo ilikutana na Ofisa Uhusiano wa hospitali hiyo, Jumaa Almasi, ambaye alisema kuwa kwa jana ilikuwa ni vigumu kuzungumzia mgomo huo kutokana na kuwa siku ya mapumziko.
“Unajua kwa (leo) yaani jana siwezi kuzungumzia mgomo kwa kuwa tuna kliniki mbili za binafsi, labda picha kamili ya kuwepo kwa mgomo tunaweza kuipata kuanzia Jumatatu, kwa vile kuna kliniki zote,” alisema.
Aidha, Ofisa Habari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha, alijikuta akishindwa kutokea katika kikao cha waandishi wa habari alichokiita ofisini kwake.

Mwananyamala na Temeke
Hali ilikuwa si shwari kwani baadhi ya wagonjwa walisikika wakisema kuwa hawajapata huduma na baadhi ya wauguzi wanajifanya kutoa huduma baada ya kuona wanahabari.
Katika Hospitali ya Amana, Tanzania Daima Jumapili ilishuhudia shughuli za matibabu zikiwa zinaendelea ingawa baadhi ya wagonjwa walikuwa wakilalamika kukaa muda mrefu pasipo kupatiwa huduma.
Mmoja wa watu waliokuwa hospitalini hapo aliyempeleka ndugu yake kupatiwa huduma baada ya kupata ajali aliliambia Tanzania Daima Jumapili kuwa wamekaa katika eneo hilo zaidi ya saa tatu bila mgonjwa wake kupatiwa matibabu.

“Nipo hapa na huyu afande tumemleta mtu aliyepata ajali maeneo ya Sitakishari lakini hatujahudumiwa mpaka saa hizi sasa sijui ndiyo wanagoma kisirisiri?” alisema mtu huyo aliyeomba jina lake lihifadhiwe.
Katibu wa utawala wa hospitali hiyo, Tunu Mwachale, alisema madaktari waliotakiwa kufika zamu kwa siku ya jana wote walifika na kwamba walikuwa wakiendelea na kazi kama kawaida.

Dk. Ulimboka anena
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Steven Ulimboka, alisema hawajapata taarifa zozote kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Kazi, ya kuzuia mgomo huo.
Alisema mgomo ulioanza jana haukihusishi Chama cha Madaktari nchini (MAT).
Alisema wao taarifa hizo wamezisikia katika vyombo vya habari hivyo hawajui kama zinawahusu wao au MAT, na kwamba itakuwa ni vigumu kutolea ufafanuzi jambo lisilowahusu.
Dk. Ulimboka alisema kuwa kimsingi serikali imekuwa ikipotosha dhana nzima ya mgomo huo kwani inaonyesha kuwa suala la posho ndilo linalogomewa na madaktari wakati si kweli.

“Watu wanadhani tunapigania posho zaidi, hapana tunapigania huduma bora kwa wagonjwa, kwa sababu sifa ya kwanza katika hospitali ya rufaa ni kuhakikisha yale yanayoshindikana katika hospitali nyingine yanawezekana katika hospitali za rufaa,” alisema.
Alitolea mfano kifaa cha kupimia cha CT- SCAN ambacho kina zaidi ya miezi saba hakifanyi kazi katika Hospitali ya Muhimbili huku ikiwalazimu baadhi ya wagonjwa wanaofika kutakiwa kufanya kipimo hicho katika hospitali nyingine.

“Wengine hawana uwezo huo, wale wanaobahatika kufika huku wanakuta kifaa hakifanyi kazi, huyu ni mgonjwa bado unamuongezea gharama nyingine, tukiyasema haya wanasema sisi hatuwajali wagonjwa,” alisema Dk. Uliomboka.
Alisema madai mengine ni pamoja na miundombinu ya hospitali kwa kile alichoeleza haziwiani na idadi ya wagonjwa na kutolea mfano wodi ya watoto katika Hospitali ya Temeke kuwa mazingira ni magumu.
Alibainisha kuwa kitaaluma ni lazima wawahudumie wagonjwa wakiwa vitandani na inapotokea wagonjwa wakiwa chini inawawia vigumu kuwahudumia, na kwamba hayo ndiyo masuala waliyokuwa wanalalamikia.
“Kwanini hospitali zetu ziwe sehemu ya mateso kwa wagonjwa badala ya kuwa sehemu ya faraja? Tunaambiwa tuwaandikie dawa wagonjwa, wakienda dirishani hata Panadol hakuna, haya hawataki kuzungumzia, wameamua kupandisha posho ya maiti wakati hata katika madai yetu hatukuwa na dai hilo,” alisema.

Matabibu asili wanena
Chama cha Utabibu wa dawa za asili Tanzania (ATME) wamewataka madaktari nchini kutopoteza uhai wa binadamu wenzao kama njia ya kuishinikiza serikali kusikiliza na kuwatekelezea madai yao.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa chama hicho, Simba Abrahaman, alisema kuwa kwa kufanya hivyo ni kuwanyima haki wagonjwa ya kupata matibabu.
Abrahaman aliwataka madaktari kukaa meza moja na serikali katika kuweza kutatua malalamiko yao na si kugoma ambapo anayeathirika ni mwananchi kwa kukosa haki hiyo ya huduma za afya.
Aidha, katika kuhakikisha mgogoro kama huo hautokei tena siku za usoni, alisema ni vema kukaundwa mfuko wa afya ambapo wananchi wataweza kuuchangia, kwa kuwa ukweli ni kwamba wamekuwa wakiitikia kuchangia mambo mbalimbali ikiwamo vyama vya siasa, hivyo halitakuwa zito.
       Chanzo cha hii habari ni Tanzania Daima la 24/6/2012 (LEO JUMAPILI)

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate