Mzee Obel Benson Mwamfupe!
Leo imetimiza miaka sita tangu baba yetu
Mpendwa ulipotutoka. Kibinadamu ni ngumu sana lakini tunamshukuru Mungu
baba wa mbinguni aliyeweza kututia nguvu na faraja tele mpaka leo hii
tuko hivi tulivyo! Tunakukumbuka kwa upendo na hekima zako.
Baba,
ulikuwa kama mti mkubwa na sisi tulikuwa kama ndege tulioweka makazi
kwako! ulipoanguka tuliyumba sana, tunazidi kumshukuru Mungu hata kwa
hili maana hajatuacha! Akatukusanya tena. Unakumbukwa na familia yako
yote wakubwa kwa wadogo. Mungu akupe pumziko la Amani.
No comments:
Post a Comment