Nani alaumiwe kwa hali hii...
Mgomo wa madaktari katika hospitali za
serikali nchini umeingia siku ya tano huku Mahakama Kuu Kitengo cha
Kazi ikimwamuru Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Namala
Mkopi, awatangazie madaktari hao wasitishe mara moja mgomo huo.
Jaji wa Mahakama hiyo, Lusekela Moshi, ametoa amri hiyo jana na kueleza kuwa Rais wa MAT anatakiwa kuwatangizia madaktari kupitia vyombo vya habari wasitishe mgomo huo hadi Julai 24, mwaka huu siku ambayo kesi ya madaktari itakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.

Alisema jalada linalowataka madaktari
kusitisha mgomo tayari limekwisha kupelekwa kwa Rais wa MAT Jumatatu
wiki hii na kwamba kinachosubiri ni rais huyo kuwajulisha wananchama hao
wasikaidi amri ya mahakama.
Jaji Moshi alisema mahakama inamtambua Rais wa MAT kuhusika katika mgomo huo kwa sababu awali alisikika akizungumza na vyombo vya habari kwamba madaktari watagoma.

Toa maoni yako juu ya huu Mgomo wa Madaktari
No comments:
Post a Comment