Wanafunzi
watano wameteketea kwa kuungua kwa moto nchini Uganda baada ya moto
kuunguza mabweni mawili ya Leos Junior Academy katika manispaa ya
Masaka.
Wanafunzi
wote waliofariki ni wa elimu ya msingi ambao wameungua hadi
kutotambulika, na miili yao imepelekwa katika hospitali ya rufaa ya
Masaka.
Kamanda
wa Polisi wa Kanda ya Kusini Simon Peter Wafana amesema tayari polisi
nchini humo imeanzisha uchunguzi wa chanzo cha moto huo.
Hii ni mara ya pili moto kuzuka katika shule hiyo katika kipindi cha miaka miwili.
No comments:
Post a Comment