Wahabeshi
21 kati ya 43 waliokufa wakivushwa katika ardhi ya Tanzania, walizikwa
leo katika makaburi ya Ipagala, manispaa ya Dodoma huku wenzao wakilia
kwa uchungu na simanzi kubwa.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Pereira Ame Silima alihudhuria maziko hayo na kutaka kuwepo kwa juhudi za pamoja za nchi za Afrika Mashariki kukomesha biashara hiyo ya kusafirisha binadamu kwani zina madhara makubwa Kitaifa na Kimataifa.
Mmoja kati ya wahabeshi waliokuwa wazima amepoteza ndugu zake watatu alionekana kuwa na dhiki kubwa kiasi cha kulazimi atafutwe mkalimani wa kumfariji.
Waziri Silima pia alitoa pole kwa wananchi wa Ethiopia ambao wamepoteza watu wao na kusema kuwa atahakikisha matukio kama hayo hayatokei tena. Akasema Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi juu ya tukio hilo na kutaka wananchi wapewe elimu zaidi ili waache biashara ya kusafirisha binadamu.

No comments:
Post a Comment