Mkuu wa shule.
Alisema kuwa wanafunzi hao walianza kuvunja vioo vya majengo na milango kisha wakaiba kompyuta 11 za shule.Mkuu huyo wa hule alisema kuwa wanafunzi hao pia walifanikiwa kuingia chumba cha kuandalia mitihani na kuchanachana mitihani yote ambayo iliandaliwa kwa ajili ya kumaliza muhula, ambayo ilipaswa kuanza jana.
Hata hivyo taarifa zaidi zinasema kuwa uongozi wa shule hiyo hauna mahusiano mazuri na wananchi wanaoizunguka shule hiyo pamoja na wanafunzi, hali ambayo wanafunzi wanadai kuwa walikuwa wakitafuta sababu ya kuanza kufanya fujo.Baada ya kupata taarifa za kuwepo na vurugu shuleni hapo, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chrispin Meela kwa kushirikiana na kamati yake ya ulinzi na usalama alifika shuleni hapo na kuzungumza na wanafunzi hao ambapo alikemea vikali kitendo hicho hicho.
Aliamua kuifunga shule hiyo hadi Julai 2, mwaka huu kwa wanafunzi wa kidato cha pili, tatu, nne na sita kwa kile alichodai kuwa walionekana kuwa ndio vinara wa uharibifu wa mali za shule.

No comments:
Post a Comment