
Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE)
Wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wa
pili wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es Salaam (DUCE), jana
walileta mtafaruku katika ofisi za Bodi ya Mikopo baada ya kuvamia
wakidai fedha za kujikimu wawapo kwenye mazoezi ya vitendo.
Wanafunzi hao ambao wako
kwenye mitihani ya kujiandaa kwenda kwenye mazoezi ya vitendo, walifika
katika bodi hiyo jana asubuhi kuishinikiza bodi hiyo kuwapatia fedha
zao.
Kutokana na uvamizi huo,
uongozi wa bodi ulilazimika kuwasiliana na polisi wilaya ya kinondoni
ili kuwasaidia ulinzi, ambapo polisi wa kutuliza ghasia walifika wakiwa
kwenye gari moja.
Kutokana na kuimarishwa kwa
ulinzi katika eneo la ofisi za bodi hiyo, wanafunzi hao walijikusanya
na kukubaliana kutuma wawakilishi wawili kuonana na uongozi wa bodi
hiyo.
Wawakilishi hao, Daniel
Amos na Vedastus Maindi, baada ya kuonana na uongozi wa bodi, walirejea
kwa wenzao kuwaeleza nini walichokubaliana.
Hata hivyo ilichukua muda
hadi wawakilishi hao kuelewana na wenzao wakati wakitoa taarifa ya nini
walichokubaliana na uongozi wa bodi.
No comments:
Post a Comment