
Mwenyekiti
wa WAMA Mama Salma Kikwete akitoa hotuba wakati wa kuzindua Kampeni ya
Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula Tanzania ambapo pamoja na mambo
mengine amesema mradi wa Fistula unalenga kumaliza tatizo la Fistula
hapa nchini ambapo inakadiriwa wastani wa Wanawake Wapya 2500 hadi 3000
hupata ugonjwa huo wakati wanapojifungua. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa
CCBRT Bw. Erwin Telemans na Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Dkt.
Wilbrod Slaa.

Mkuu
wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema akisoma hotuba kwa niaba ya Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam katika uzinduzi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa
matibabu ya Fistula Tanzania.

Mkurugenzi
Mkuu wa CCBRT Bw. Erwin Telemans akizungumza katika uzinduzi huo ambapo
amewataka Wanawake kujitokeza kupatiwa matibabu kwa kuwa tunataka
Tanzania bila FISTULA na kusisitiza tuwe mfano wa kuigwa na nchi zingine
katika kutokemeza ugonjwa huu.

Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Bw. Michael John akitoa
hotuba kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo ambapo amesema Serikali ya
Tanzania iko bega kwa bega na CCBRT pamoja na wadau wengine katika
kuhakikisha lengo la kutokomeza Ugonjwa wa FISTULA linatimia.

Mwenyekiti
wa WAMA Mama Salma Kikwete (wa pili kulia) akipitia hotuba huku
Mkurugenzi Mkuu wa CCBRT Bw. Erwin Telemans (kushoto) akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Dkt. Wilbrod Slaa. Kulia ni Mkuu wa Wilaya
ya Temeke Bi. Sophia Mjema.

Shuhuda
Beatrice Ramadhani na mumewe Hosea Wilson Sanga akisimulia jinsi
alivyopatwa na ugonjwa wa FISTULA na kupoteza mtoto wa kwanza lakini
alipopata taarifa kuwa ugonjwa huo unatibika alifika katika Hospitali ya
CCBRT na kupatiwa matibabu bure na sasa amepona kabisa na kufanikiwa
kupata mtoto.

Bw.
Hosea Wilson Sanga akizungumza ambapo amewaasa kina baba kutowatenga
wake zao wanapokuwa na ugonjwa wa FISTULA na badala yake ni kuwapa moyo
na kwapeleka Hospitali kwa ajili ya matibabu.

Mama Salma Kikwete akimpongeza Shuhuda Beatrice Ramadhani kwa ujasiri wa kujitokeza na kuwa mfano kwa wanawake wengine.

Wasanii
wa Kikundi cha Mjomba Bendi wakionyesha igizo lenye fundisho kwa
wanaume kutowafukuza wake zao majumbani wanapougua ugonjwa wa FISTULA
kwa kuwa Ugonjwa huo husababisha Mwanamke kushindwa kudhibiti haja ndogo
na kubwa.

Msanii
wa kughani mashairi Mrisho Mpoto akiwasilisha Ujumbe kwa jamii nini cha
kufanya pindi wanapoona mwanajamii mwenzao anaugua ugonjwa wa FISTULA.

Mwenyekiti
wa WAMA Mama Salma Kikwete akielekea kujumuika kuserebuka na wananchi
sambamba na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kulia).



Mwenyekiti
wa WAMA Mama Salma Kikwete (kulia) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi
rasmi wa Kampeni ya Uhamasishaji wa Matibabu ya FISTULA itakayoendeshwa
nchi nzima ambapo wanawake wanaougua Ugonjwa huo watapata matibabu
Bure. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mipango ya Kijamii wa CCBRT
Brenda Msangi (katikati) na Meneja Mawasiliano wa CCBRT Bw. Abdul
Kajumulo.

Dkt.
Willbrod Slaa akitoa neno la Shukrani kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kwa mchango wake katika
kuhakikisha kampeni hii inafanikiwa.

Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa umakini Mwenyekiti wa Bodi ya CCBRT Dkt. Wilbrod Slaa (hayupo pichani).
Pichani Juu na Chini ni baadhi ya Wafanyakazi wa CCBRT na Wananchi waliofika viwanja vya Mnazi Mmoja kushuhudia uzinduzi huo.
Bw. Abdul Kajumulo (kushoto) akiwa na Wafanyakazi wenzake wakihakikisha zoezi zima linakwenda sawa.
Wanawake
kote nchini wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Fistula wametakiwa kutojificha
kwa kuogopa aibu, badala yake wajitokeze na wafike hosptali kupatiwa
matibabu kwa kuwa ugonjwa huo unatibika.
Rai
hiyo imetolewa leo na Mama Salma Kikwete wakati akizindua Kampeni ya
Uhamasishaji wa Matibabu ya Fistula ambapo amesema miongoni mwa athari
za ugonjwa huo ni mama kupoteza kichanga wakati wa kujifungua, kupoteza
uwezo wa kudhibiti haja ndogo na/au kubwa na kutokwa na haja ndogo na
kubwa kwa wakati mmoja, kupitia njia moja.
Mama
Salma amesema ugonjwa huo ni moja ya changamoto katika sekta ya afya
hapa nchini na hivyo akatoa wito kwa taasisi binafsi na mashirika na
wadau wa maendeleo na wananchi kwa ujumla kujitoa kusaidia juhudi za
kutokomeza tatizo hili la Fistula.
Chanzo cha habari Na.MO BLOG TEAM




No comments:
Post a Comment