Petr Jiracek alifunga bao la
pekee katika mechi ya uwanja wa Wroclaw dhidi ya wenyeji Poland siku ya
Jumamosi, na kuwahuzunisha mashabiki wa nyumbani, wakati Jamhuri ya
Czech ilipofuzu kuingia robo fainali za mashindano ya Euro 2012.
Jamhuri ya Czech imefuzu katika kundi hilo, baada ya kuongoza kwa pointi 6.
Jiracek, kiungo cha kati wa timu ya Wolfsburg ya
Ujerumani, aliweza kuutambariza mpira wavuni katika sehemu ambayo kipa
Przemyslaw Tyton hakuweza kuwa na matumaini kabisa ya kuufikia mpira,
zikiwa zimesalia dakika 18 tu mechi hiyo kumalizika.
Poland walianza mechi wakifahamu kwamba iwapo
wangelipata ushindi katika mechi hiyo, basi wangeliweza, kwa mara ya
kuwanza, kuwa miongoni mwa timu nane ambazo zingelisalia katika
mashindano kushiriki katika mechi za robo fainali.
Nahodha wa Poland Jakub Blaszczykowski, katika
juhudi za dakika ya mwisho alikuwa nusra afunga bao la kusawazisha,
lakini ulinzi wa Czech ulikuwa thabiti, na mpira kuondolewa kabla ya
kuvuka msitari.
No comments:
Post a Comment