Serikali imewaachisha kazi rasmi wafanyakazi 398 wa Mgodi wa Makaa ya
Mawe wa Kiwira mkoani Mbeya na kuukabidhi mgodi huo kwa Shirika la Taifa
la Madini (STAMICO) kwa uendelezaji zaidi.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, alisema uamuzi huo wa kuwasimamisha kazi wafanyakazi hao umefikiwa na Baraza la Mawaziri na kwamba taratibu zote za malipo yao ziko kwenye hatua za mwisho.
“… hili limefanyika kwa taratibu zote huku Chama cha Wafanyakazi hao kikishirikishwa na hadi kufikia Julai 9, mwaka huu, wafanyakazi wote watalipwa mafao na stahili zao,” alisema Maswi.
Alisema mwaka 2005 Serikali iliingia ubia na Kampuni ya kizalendo ya Tan Power Resources (KCPL) ambapo Serikali ilikuwa na hisa asilimia 30 huku KCPL asilimia 70, kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe, lakini kampuni hiyo ilishindwa kuuendeleza mgodi huo.
Alisema Serikali baada ya kuona kampuni hiyo imeshindwa kuuendeleza mradi huo, iliurejesha kwake na ilikabiliana na majukumu ya kulipa malimbikizo ya wafanyakazi wa mgodi huo na madeni yake ya nyuma.
Alisema kuanzia mwaka 2008, Serikali ilipourejesha mgodi huo mikononi mwake, iliwalipa mishahara na malimbikizo wafanyakazi hao 398 yanayofikia Sh. bilioni 4.5 ambao wakati huo walikuwa hawafanyi kazi yoyote ya msingi, na fedha nyingine, Sh. bilioni 32 zililipia madeni ya mikopo ya mradi huo.
via HabariLeo

No comments:
Post a Comment