EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, July 21, 2012

Mfanyibiashara Arusha anashikiliwa kwa kumuoa mtoto wa miaka 8 na kumpa ujauzito

Mfanyabiashara aliyetambulika kwa jina la Joseph Ngisha (24) mkazi wa Sakina, Songambele, jijini Arusha anashikiliwa na polisi kwa kosa la kumuoa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 kinyume cha sheria kwa mahari ya ng'ombe wanne.

Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, polisi pia inamshikilia baba mzazi wa mtoto huyo, Lemomomo Olokuto (42) mkazi wa Mto wa Mbu kwa tuhuma za kumwoza mtoto wake tangu mwaka 2010 akiwa na miaka 8 (sasa hivi mtoto huyo ana umri wa miaka 11.)

Alisema Ngisha alitiwa mbaroni Julai 18, mwaka huu majira ya saa 3.45 asubuhi nyumbani kwake baada polisi kupata taarifa za siri na kumkuta akiishi na mtoto huyo huku akiwa amembebesha ujauzito wenye umri wa miezi mitatu.

''Ngisha alipohojiwa na polisi alikiri na kueleza kuwa yeye alitoa mahari ya ngómbe 4 badala ya 3 waliotajwa na baba mkwe wake'' alisema.

Kamanda Sabas alifafanua kuwa Ngisha alianza kumchumbia mtoto huyo baada ya kuacha  kunyonya kwa mama yake na kwamba alipofikisha umri huo aliwafuata wazazi wake na kuwaeleza nia ya kutaka kumchumbia.

Hata hivyo, mzazi wa upande wa mama  aligoma huku baba yake ambaye ni mtuhumiwa akiruhusu mtoto wake aolewe bila kupingwa.

Aliongeza kuwa, mtuhumiwa Ngisha baada ya kuona mama mzazi akipinga mtoto wake asiolewe, alimrubuni  kuwa anakwenda kumsomesha shule, kitendo ambacho hakukifanya na badala yake alikuwa akimwingilia kimapenzi na kumfanya kama mkewe.

Kamanda alisema  kuwa taarifa za mtuhumiwa kuishi na mtoto huyo kama mke ziligunduliwa na majirani kwani mara nyingi alikuwa akimfungia ndani bila mtu kujua huku akiwaeleza baadhi ya jamaa zake kuwa ni mdogo wake.

Aidha, alisema kuwa kwa sasa mtoto huyo yupo chini ya uangalizi wa ofisi za ustawi wa jamii jijini Arusha, ambapo anachunguzwa kiwapo atakuwa  ameathirika na magonjwa ya zinaa ama la.

Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtoto huyo ameathiriwa kwa kupata ujauzito wa miezi mitatu ambapo kulingana na umri wake ni vigumu kuhimili maisha ya kuitwa Mama.

Baba wa mtoto huyo alipoulizwa alikiri kumwoza mtoto wake kwa mahari ya ngómbe watatu tofauti na idadi  inayotajwa na mkwewe Ngisha.

Uchunguzi wa awali kutoka ndani ya jeshi la polisi unaonyesha kuwa Ngisha alimchukuwa mtoto huyo tangu mwaka 2010, hata na hivyo alipohojiwa kwa mara ya kwanza aklikataa kosa hilo hadi siku ya jana ambapo alikiri kutenda kosa hilo.

Sabas alisema kuwa kufuatia tukio hilo, baba mzazi anashikiliwa na kumuunganisha na Baba mkwe wake, na kwamba wote wawili watafikishwa mahakani kujibu tuhuma zianzowakabili baada ya jeshi la polisi mkoani Arusha kukamilisha uchunguzi wake kuhusiana na tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate