Mtoto mwenye vichwa viwili
MKAZI wa Mtaa wa Chiringe, katika mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, Sarah Abidenego amejifungua mtoto akiwa na vichwa viwili.
MKAZI wa Mtaa wa Chiringe, katika mamlaka ya mji mdogo wa Bunda, Sarah Abidenego amejifungua mtoto akiwa na vichwa viwili.
Akizungumza na jana katika wodi ya wazazi katika
Hosptali ya DDH iliyoko mjini hapa, mwanamke huyo alisema alipokuwa
mjamzito alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo na kwamba Julai 24
majira ya saa 3:45 alijifungua mtoto wa kike akiwa na vichwa viwili.
Akielezea suala hilo, muuguzi wa zamu katika wodi hiyo, Sophaleti
Majanjala, alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 1.9 na
kwamba baada ya kuzaliwa alikaa muda wa saa moja na kufariki dunia.
“Huyu mtoto baada ya kuzaliwa aliishi kwa muda mfupi kama saa moja
hivi na baadaye alifariki dunia , tunasubiri baadaye tuwakabidhi maiti
kwa ajili ya kwenda kuzika,” alisema muuguzi huyo.
Mwanamke huyo alisema anamshukuru Mungu kwa kuwa ndiye aliyempa kiumbe
hicho na pia ndiye aliyekichukua na kwamba ana matumaini atabeba mimba
nyingine na atazaa mtoto aliye na viungo vilivyokamilika, kwani hiyo
ilikuwa ni mimba yake ya kwanza.
Alifafanua kuwa wakati akiwa na ujauzito huo hakupata shida ya
kuuguaugua mara kwa mara, lakini wakati wa kujifungua alishangaa kuona
anajifungua mtoto akiwa na vichwa viwili.
Tukio hilo lilivuta hisia za watu wengi ambao walifika katika wodi
hiyo kutaka kukiona kichanga hicho, lakini kwa bahati mbaya walikuta
tayari kimeshafariki dunia, hivyo hawakuruhusiwa kukiona.
No comments:
Post a Comment