Mtoto Isack Hamis Suluhu (5),
amefariki dunia na wengine saba wamenusurika baada ya jahazi walilokuwa
wakisafiria kutoka Pemba kwenda Unguja kuzama katika Bahari ya Hindi.
Tukio hilo limekuja wiki moja tu tangu boti ya MV Skagit ilipopinduka na kuzama katika mkondo wa Chumbe na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 100.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kusini Pemba, Hassan Ali, alisema jahazi hiyo inayojulikana kama Safina ilizama katika eneo la mkondo wa Nungwi juzi jioni.
Alisema kati ya walionusurika mmoja hali yake ni mbaya na amelazwa katika hospitali moja mjini Pemba na kwamba wengine saba wakiwemo watoto wawili hali zao ni nzuri.
Kamanda Ali alisema chanzo cha ajali hiyo ni kujaza mizigo na abiria wengi kupita uwezo wake na kwamba watu hao kwa kuwa ni wazoefu na shughuli za uvuvi walijiokoa wenyewe kwa kuogelea.
Kumekuwa na mfufulizo wa matukio ya meli na jahazi kuzama katika Bahari ya Hindi hali ambayo inatishia usalama wa maisha ya watu wanaotumia usafiri wa majini.

No comments:
Post a Comment