EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Friday, July 13, 2012

Ndoa ya Slaa njia panda: MAHAKAMA Kuu imepanga kuanza kusikiliza kesi ya kupinga ndoa ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na mchumba wake Josephine Mushumbusi Agosti 14


Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Ester Bulaya wakimpongeza Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Rose Kamili (kulia) katika Viwanja vya Bunge jana baada ya kupata taarifa kuwa Rose amefungua kesi ya kuzuia ndoa ya aliyekuwa mumewe, Katibu Mkuu wa Chadema,Dk Willibrod Slaa inayotarajiwa kufungwa Julai 21. Picha na Edwin Mjwahuzi
WAKILI WAKE ASEMA HAKUNA ZUIO LA MAHAKAMA, JAJI KUSIKILIZA KESI AGOSTI 14

MAHAKAMA Kuu imepanga kuanza kusikiliza kesi ya kupinga ndoa ya Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa na mchumba wake Josephine Mushumbusi Agosti 14, mwaka huu.Slaa na Mushumbusi walitarajia kufunga ndoa katika Kanisa Katoliki Julai 21, mwaka huu, lakini Rose Kamili, anayedai kuwa ni mke wa Dk Slaa, amefungua kesi kuipinga na kudai fidia ya Sh550 milioni.Jana, Jaji Lawrance Kaduli akitaja kesi hiyo namba 4 ya mwaka 2012, alisema Dk Slaa na Mushumbusi wanatakiwa kujibu pingamizi hilo la ndoa kwa njia ya maandishi kabla ya Julai 30, mwaka huu.

Pia alimtaka Kamili kupitia wakili wake, Joseph Thadayo kama watakuwa na majibu yoyote wayasajili Agosti 7, mwaka huu na baada ya taratibu hizo Agosti 14, mwaka huu atasikiliza kesi hiyo.

Kitendo cha kesi hiyo kupangiwa tarehe ya mbele, siku 22 baada ya siku iliyopangwa kwa ajili ya kufunga ndoa, kinaiweka ndoa ya wawili hao njia panda na kuacha maswali mengi iwapo itafungwa au la.Mutakyimilwa Philemon ambaye ni wakili wa Dk Slaa alipoulizwa nje ya mahakama kuhusu mchakato huo wa kisheria kama utazuia ndoa hiyo kufungwa, alijibu:

“Hakuna amri ya mahakama ya kuzuia ndoa. Kwa hiyo itategemea busara tu. Lakini, sitaki kuzungumza kama ndoa ipo au haipo, hilo ni jambo la mahakamani.”

Madai ya Kamili
Katika kesi hiyo, Kamili ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), anaiomba mahakama kusimamisha ndoa hiyo.
Pia anaiomba mahakama iamuru Dk Slaa amlipe Sh50 milioni kama fidia ya fedha alizotumia kujihudumia pasipo matunzo ya mumewe.
Mbunge huyo pia anaiomba mahakama iamuru Mushumbusi amlipe Sh500 milioni kama fidia ya maumivu aliyoyapata kutokana na kitendo chake cha kuingilia ndoa yao.

Katika hati hiyo ya madai, mbunge huyo anadai kuwa ndoa inayotarajiwa kufungwa kati ya Dk Slaa na Mushumbusi ni batili kwa sababu kuna ndoa nyingine halali na inayoendelea kuishi, kati yake na mumewe huyo iliyofungwa mwaka 1985.
Alidai baada ya kufungwa kwa ndoa hiyo, Juni 18, mwaka 1987 walifanikiwa kupata mtoto wa kike anayeitwa Emiliana Muchu na baadaye Septemba 23,  mwaka 1988 walipata mtoto mwingine wa kiume, Linus Amsi.

Anadai kuwa katika uhusiano wao, Slaa akiwa ni Padri alifanya taratibu zilizomwondosha katika nafasi hiyo ya upadri na kuanza maisha ya familia.
Baada ya taratibu hizo, anadai kuwa jamii ya Watanzania iliwatambua kama mume na mke, na hata kumbukumbu za hati za kimataifa kama za kusafiria ziliwatambua kuwa wanandoa.

Kamili aliendelea kudai katika maelezo hayo kuwa, yeye na Slaa waliishi maisha ya ndoa yenye amani, yaliyowawezesha kupata mali kadhaa walizomiliki kwa pamoja ikiwamo nyumba iliyopo kwenye kiwanja namba 609 kitalu E, nyumba ya makazi iliyopo katika Kijiji cha Gongali, Karatu na vifaa mbalimbali vya nyumbani.

Hati ya mashtaka imeendelea kueleza kuwa, uhusiano kati ya Slaa na Kamili, ulianza kuharibika mwaka 2009, baada ya Slaa kuwa na uhusiano na mwanamke mwingine kinyume cha sheria.

"Tangu mwaka 2009, Slaa akaitelekeza familia yake kwa kutoipatia huduma," imeeleza hati hiyo.
Kamili anaiomba mahakama iamuru kuwa yeye na Slaa bado ni mke na mume na kwamba, Mushumbusi aliingilia ndoa yao, hivyo mahakama izuie ndoa inayotarajiwa kufungwa Julai 21, mwaka.

Kamili pia amewasilisha hati hiyo ya mashtaka kwa Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki nchini, Mwadhama Polycarp Kadinali Pengo.
Kamili amemweleza Kadinali Pengo ambaye pia anaongoza Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, kuwa moja ya Parokia za Dar es Salaam zina taarifa ya ndoa hiyo.

Nakala ya madai hayo pia imewasilishwa kwa Msajili wa Mahakama Kuu, Msajili wa Ndoa na kwa Askofu wa Jimbo la Mbulu.
Via Gazeti la mwananchi

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate