MWIGIZAJI na Mtayarishaji wa filamu za
Swahiliwood, Juma Kilowoko Sajuki ameiambia Mwanaspoti kuwa hali
aliyoondoka nayo Tanzania kwenda India ilikuwa mbaya na kila alipopatiwa
dawa haikusaidia.
Hali haikuwa nzuri, maumivu niliyokuwa nayapata kama ningeliendelea kusubiri zaidi ya wiki moja tu hapa kwa kweli mngenisahau," alisema.
"Nilikuwa naumwa sana, lakini pia jambo lingine ilikuwa hizo gharama za matibabu kuwa juu wakati mimi pamoja na mke wangu kwa muda mrefu hatukuwa tunazalisha kutokana na kuumwa kwa kipindi kirefu."
Sajuki anawashukru madaktari waliomtibia nchini India akisema tangu alipowasili alipokewa kwa ukarimu na kushughulikiwa kwa haraka.
"Unajua nilipoondoka hapa sikuwa na uwezo hata wa kula, lakini baada ya siku chache pale nikaanza kula vizuri na kuwafurahisha madaktari. Huduma pale ni ya gharama kubwa lakini anashukuru," aliongeza.
Msanii huyo amerudi salama na anaendelea na vizuri japo kuna dawa ambazo anaendelea nazo. Baada ya kukusanya nguvu atarudi tena India kwa ajili ya matibabu zaidi.Via Mwanasport.

No comments:
Post a Comment