Serikali ya Zanzibar imetoa msimamo wake wa kutokukubaliana na baadhi ya
taasisi za dini zinazowahamasisha waumini wake kutoshiriki katika zoezi
la sensa ya watu na makazi litakalofanyika tarehe August 26 Mwaka huu.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesea hayo wakati akifungua rasmi mafunzo ya wakufunzi wa zoezi la sensa ya watu na makazi huko Tunguu Kisiwani Unguja na kusema kuwa lengo la Serikali ya Muungano na ile ya Zanzibar ni kuona watu wote wanahesabiwa pasipo kubagua dini ama kuona taasisi fulani inajitenga kwa vigezo fulani ambavyo amesema kiundani havina mantiki ya kutoshiriki zoezi hilo.
Tanzania inatarajia kutekeleza zoezi la sensa ya watu na makazi ambalo huja kila baada ya miaka kumi ili kuwezesha serikali kupanga mipango yake ya kimaendeleo kikamilifu kulingana na idadi ya watu waliopo nchini.
Naye mtakwimu mkuu wa sense Zanzibar ameiomba serikali kulijadili swala la kidini kwa undani ili watu wote wahesabiwe katika zoezi hilo kwani wasipohesabiwa nchi ndiyo itakayoathirika na sio taasisi ya kidini.
Hajji Bwegege, TBC Zanzibar.

No comments:
Post a Comment