Afisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp
Limited, Hussein Mbululo (kulia) akifafanua jambo juu ya Tuzo ya Dhahabu
waliyo ipata kutoka Geneva Uswis kwa Ubora wa huduma zao, kwa waandishi
wa Habari waliotembelea banda la Benki hiyo katika maonesho ya
kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yanayoendelea katika viwanja vya
JK Nyerere maarufu Saba Saba barabara ya Kilwa. Pamoja ni wafanyakazi wa
Benki hiyo waliopo viwanjanani hapo.
SIKU chache baada ya kupokea Tuzo ya
dhahabu ya Kimataifa ya utoaji bora wa huduma, Benki inayomilikiwa na
Serikali ya Twiga Bancorp, imeweka hadharani siri ya kupewa tuzo hiyo
inayojulikana kama Century International Gold Quality ERA.
Benki ya Twiga Bancorp ilikabidhiwa
tuzo hiyo karibuni na Kampuni ya Kimataifa ya Business Initiative
Directions jijini Geneva Uswis.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Hussein Mbululo, alisema huduma ya
moneygram inayowezesha Watanzania na watu wa mataifa mengine kutuma
fedha nje kwa dakika chache imechangia kuiwezesha benki hiyo kushinda
tuzo hiyo.
Tuzo hiyo kwa Benki ya Twiga Bancorp
imekuja siku chache baada ya Serikali kupitia kwa Waziri wa Fedha na
Uchumi, Dk. William Mgimwa kuliambia Bunge kwamba Serikali ipo mbioni
kuziongezea mtaji benki zake ikiwemo Benki ya Twiga ili kuziwezesha
kuboresha huduma zake. Benki nyingine ni Benki ya Wanawake (TWB), Benki
ya Posta (TPB) na Benki ya Rasilimali (TIB).
Mbululo alisema huduma nyingine
iliyoiwezesha benki hiyo kushinda tuzo hiyo ni utoaji wa mikopo kwa
wafanyakazi bila kuwalazimu wafanyakazi hao kuwa na akaunti katika Benki
ya Twiga hatua ambayo imewezesha wafanyakazi nchi nzima hata mahali
kusiko na benki hiyo kunufaika na mikopo hiyo.
“Walieleza kuridhishwa na huduma zetu
kufikia kiwango cha ubora wa juu lakini pia walieleza kuridhishwa na
ubunifu tunaoendelea kuufanya katika kuboresha huduma za kibenki nchini
ukilinganisha na benki nyingine.
Kupitia huduma za Money gram mtu
anaweza kumtumia fedha za ada au dawa kwa mwenzake aliyepo Uingereza au
Marekani na akaweza kuzipata ndani ya dakika tano tu jambo ambalo
limewavuta watu wengi kutumia benki yetu,” alisema Mbululo.
Alisema benki hiyo pia imetoa mchango
mkubwa katika maendeleo ya Benki Kata za Jamii (VICOBA) katika maeneo
mbalimbali hapa nchini hatua ambayo imewezesha kupewa nishani ya kuwa
mlezi bora wa VICOBA nchini na kupewa tuzo.Hadi sasa Benki hiyo
inahudumia vikundi zaidi ya 150 vya VICOBA.
Alisema benki hiyo inayoendelea
kujitanua kwa kufungua tawi moja mkoani kila mwaka, hivi karibuni
itafungua tawi jipya mkoani Dodoma na hivyo kuifanya kuwa na matawi Dar
es Salaam, Arusha, Mwanza na Dodoma, huku tawi la Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Dar es Salaam, likiendelea kuvunja rekodi ya kufunguliwa
kwa saa 24 kwa siku zote saba za wiki.
Alisema mtandao wa huduma kwa benki
hiyo umeimarika kutokana na kadi zake za ATM kuweza kuunganishwa na
Mtandao wa Umoja wenye kuzihusisha benki zaidi ya 24, zikiwa na mtandao
wa zaidi ya ATM 160 nchi nzima.
Kuhusu mtaji utakaongezwa na serikali
kwa benki hiyo, Mbululo alisema fedha hizo zitasaidia kuboresha huduma
za benki hiyo kwa kuwezesha kujenga matawi mapya, kununua mashine na
kununua kompyuta na vifaa vyake ili kutanua zaidi huduma zake na
kuwezesha kuwafikia wananchi wengi.
Afisa Mwandamizi, Mwendeshaji, Lydia
Matembele akitoa maelezo kwa vijana waliotembelea banda lao katika
maonesho ya Kimaifa ya Biashara maarufu saba saba .
Banda la Twiga Bank lipo kando ya lango kuu la Kuingilia Karume Hall.
Benki ya Twiga Bancorp inatoa huduma
ya kuweka na kuchukua fedha dirishanai au katika ATM yake iliyopo
viwanja vya Sabasaba kama mmoja wa wateja wa Umoja Switch anavyofanya.
Mkuu wa Uendeshaji Richard Kombole (kulia)akizungumza na mteja nje ya Banda lao
Afisa Mwandamizi, Mwendeshaji, Lydia
Matembele akimsikiliza Mfanya Biashara, Yahia Idriss wa Kampuni ya Giad
Sewedy Cables ya Nchini Sudan alipofika kupata huduma ya kubadilishiwa
fedha katika Banda hilo la Maonesho linalofanya huduma kamili za
Kibenki.
No comments:
Post a Comment