
Sauda
Mwilima mtangazaji wa Star Tv
Baada
ya kubeba ujauzito na baadaye kujifungua watoto wasio riziki, mstaa wa
Tanzania, Ndumbangwe Misaya a.k.a Thea na mwenzake, Sauda Mwalima ambaye ni
mtangazaji wa Star Tv wadau mbalimbali wamewapa pole wazazi hao.
Watu
waliomwaga pole hizo kupitia mtandao huu walisema taarifa za kujifungua
hatimaye watoto wao wakawa siyo riziki ziliwashtua sana kwa vile ni wao wenyewe
waliamini kinyume cha hapo.
“Unajua
unaposikia mama aliyelea mimba yake kwa miezi tisa bila matatizo, unapokuja
kujsikia amejifungua lakini amepoteza mtoto huyo inauma sana. Kwani inamaanisha
kwamba miezi yote tisa aliyojitahidi kulea ilikuwa kazi bure na mategemeo yake
yamepotea,” mama Rubein ambaye ni mkazi wa Ilala alisema.
Sauda
Mwilima, alijifungua mtoto si riziki miezi michache tu baada ya kufunga ndoa. Kinachouma
zaidi ni kwamba mtangazaji huyo alijifungua kwa kufanyiwa upasuaji na siku za
karibuni aliripotiwa yupo nyumbani anaendelea kuuguza majeraha yake.
Thea ambaye
mumewe ni staa wa movie za Tanzania, Michael Sangu ‘Mike’ nay eye pia
alijifungua baada ya kuishi miaka miwili katika ndoa lakini kwa bahati mbaya
sana mtoto wake akapoteza maisha.

No comments:
Post a Comment