WAZIRI wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Dkt. Hawa Ghasia, ametoa siku 21 kwa Ofisa Utumishi wa
Wilaya ya Sengerema, Mkoani Mwanza Bw. Lusajo Ngabo, kuwalipa walimu
400 wa wilaya hiyo wanaodai malimbikizo ya mishahara yao.
Hatua hiyo imekuja baada ya Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Wilayani Sengerema Bw. Joseph Mashinji, kuomba ufafanuzi kwa Waziri kuhusu kuchelewa kwa fedha za walimu, wakati wa kikao cha watumishi wa Halmashauri ya Sengerema, Julai 3, Mwaka huu.
Waziri Ghasia alisema suala la kucheleweshwa kwa malipo ya watumishi na kusababisha malimbikizo ya madai siyo la wizara ya utumishi, bali ni uzembe wa Maoafisa utumishi katika, Halmashauri hiyo.
Alisema kuwa malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma yamesababisha baadhi ya watumishi katika idara mbalimbali hususan, Elimu na Afya kufikia hatua ya kuanzisha migomo isiyo na tija katika Taifa, kutokana na ucheleweshwaji wa taarifa za watumishi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo, aliyekuwa mwenyeji wa Waziri Ghasia Mkoani Mwanza, aliwaambia watumishi kuwa wavumilivu wakati Ofisa Utumishi wa Sengerema, Bw. Ngabo akiendelea na zoezi hilo.
Katika hatua nyingine Waziri Ghsia alisema, TAMISEMI, imeanzisha mfumo wa Lawson, yaani mfumo unaopokea mshahara na kuwachukulia hatu pamoja na kusaidia kutuma taarifa za watumishi katika ngazi za halmashauri za wilaya na kwamba mfumo huo tayari umeanza kutekelezwa kuanzia mwezi Januari mwaka huu katika halmashauri zote nchini.
Waziri Ghasia alikuwa na ziara ya siku mbili katika Mkoa wa Mwanza kwa lengo la kuzungumza na Wakuu wa idara, Madiwani na Watumishi wa halmashauri za Wilaya ili kuwakumbusha nia ya Serikali katika kusimamia maendeleo.
Nyakasagani,
OFISA UTUMISHI SENGEREMA APEWA SIKU 21

No comments:
Post a Comment