Waziri Mkuu akiwasili katika uwanja wa ndege wa Musoma tayari kuelekea Kijijini Busegwe kwa mazishi
Waziri Mkuu akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Mara wa Vyama na Serikali
Kaburi la Mwalimu James Irenge aliyezaliwa mwaka 1892 na kufariki 2012
Waziri Mkuu Mizengo Pinda hii leo amewaongoza maelfu ya wakazi wa
Mkoa wa Mara katika Mazishi ya Mwalimu James irenge aliyemfundisha Baba
Wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1935 katika Shule ya Msingi
Mwisenge iliyoko katika Manispaa ya Musoma. Marehemu Mwalimu Irenge
amezikwa leo katika kijiji alichozaliwa cha Busegwe Nyanza, Wilayani
Butiama kwa heshima zote za Kiserikali.
Marehemu alizaliwa mwaka 1892 katika kijiji cha Busegwe, mwaka
1924-1925 alisoma Standard two Busegwe, Mwaka 1927 alisoma darasa la
pili, Mwisenge middle school, Mwaka 1932 alijiunga na Chuo cha Ualimu
Mpwapwa, 1934 alifundisha Chuo cha Ualimu Mpwapwa, 1935 alihamia Shule
ya Msingi
Mwisenge ambapo alikutana na Hayati Baba wa Taifa na
kumfundisha darasa la tatu na la nne akiwa anaishi naye Mtaa wa
Mkinyerero, Mwisenge. Marehemu alistaafu mwaka 1970 akiwa mkaguzi wa
Shule za Msingi katika Wilaya za Geita na Biharamuro.
Baada ya kustaafu Hayati Baba wa Taifa alimshauri aanzishe Kijiji cha
Ujamaa ambacho kiliitwa Ihayabuyaga huko Geita, Mwanza. Mwaka 1980
alirejea nyumbani kwake Mwisenge. Marehemu ameacha Mjane, watoto kumi na
wajukuu 35, vitukuu 4 na vilembwe wawili.
Paschal Michael, Musoma.
www.wotepamoja.com
www.wotepamoja.com
No comments:
Post a Comment