MABINGWA watetezi Yanga watakutana na Azam katika fainali ya Kombe la Kagame kesho baada ya timu hizo kuzifungashia virago APR ya Rwanda na AS Vita ya DR Congo katika mechi za nusu fainali zilizofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga iliwalazimu kusubiri hadi dakika ya100 kupata ushindi wake wa bao 1-0 dhidi APR kwa goli la Hamis Kiiza aliyefunga kwa kifua akiunganisha krosi ya Haruna Niyonzima, huku Azam ikiwafungashia virago AS Vita kwa mabao 2-1 shukrani kwa mabao ya John Bocco na Mrisho Ngasa.
Kwa matokeo hayo sasa Kombe la Kagame linabaki Tanzania kwa mara ya pili mfululizo baada ya mwaka jana Yanga kucheza fainali na Simba.
Fainali ya kesho itakuwa na
utamu wa aina yake kutokana na upinzani wa Yanga na Azam uliozaliwa
Machi10 mwaka huu ambapo mabingwa hao watetezi wa kombe la Kagame
walichapwa 3-1 na kuishia kumpiga mwamuzi Israel Nkongo na kusababisha
baadhi ya nyota wake kufungiwa.
Yanga waliingia kwenye mchezo huo kwa kishindo na dakika ya kwanza shuti la Kiiza lilidakwa na kipa wa APR Ndoli Jean Claude.
APR walijibu mapigo na dakika ya 7 shuti la Leonel Preus liligonga mwamba na kurudi uwanjani, huku shuti la umbali wa mita 30 la Athuman Idd likipanguliwa kwa ustadi mkubwa na kipa Ndoli Jean na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.
Pia kipa wa Yanga, Ally Mustapha alifanya kazi nzuri kupangua shuti la Dan Wagaruka na kuwa kona ambayo iliokolewa na mabeki wa Yanga.
Katika kipindi cha kwanza mwamuzi wa mchezo huo Anthony Ogwayo kutoka Kenya alitoa kadi za njano kwa Shamte Ally, Kiiza na Godfrey Taita kwa makosa tofauti.
Yanga iliingia kipindi cha pili kwa kasi zaidi na kuanza kufanya mashambulizi ya nguvu langoni mwa APR ambao walionekana kuanza kuchoka na kuondoka mchezoni kila dakika ilivyokuwa ikiendelea kupita.
Katika kipindi cha pili APR walimtoa Preus na kumwingiza Mubumbyi Barnabe wakati Yanga walimtoa Shamte na kumwingiza Rashid Gumbo mabadiliko yaliyokuwa na faida kwa mabingwa hao watetezi.
Mchezo huo ulimaliza dakika 90 huku matokeo yakiwa 0-0 na hivyo mwamuzi wa mchezo kulazimika kuongeza dakika 30.
Ilipofika dakika ya 99, Bahanuzi alifanyiwa faulo na wachezaji wawili wa APR pembeni ya uwanja na mpira kutoka nje, ambapo wakati wachezaji wa APR wakimlaumu mchezaji huyo kwa kujiangusha na kusubiri maamuzi ya mwamuzi, Yanga walirusha mpira kwa haraka na kumkuta Haruna Niyonzima aliyeingia kwa kasi na kupiga krosi iliyomkuta Kiiza aliyeusukuma mpira wavuni kwa kifua dakika katika dakika ya100.
Kuingia kwa bao hilo kuliamsha shangwe kwa mashabiki wa Yanga waliojitokeza kwa wingi uwanjani hapo.
Hakuna ushindi usiokuwa na kilio ndicho kilichotokea uwanjani hapo baada ya beki wa Yanga, Taita kuonyeshwa kadi ya pili ya njano na kutolewa nje kwa kadi nyekundu katika dakika ya103.
Kutolewa kwa beki huyo kuliwalazimu Yanga kucheza dakika 20 wakiwa pungufu kulinda ushindi wao huo na hadi filimbi ya mwisho inapulizwa walitoka kifua mbele kwa ushindi wa bao 1-0.
Katika mechi ya awali, Azam walilazimika kusawazisha bao kabla ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Vita na kufuzu kucheza fainali ya Kombe la Kagame kwa mara ya kwanza.
Mshambuliaji John Bocco wa Azam alifunga bao lake la tano kwa kichwa kwenye mashindano hayo akisawazisha lile la mapema lililofungwa na Mfogang Alfred wa Vita kwa shuti kali akiwa nje ya 18 kabla ya Mrisho Ngasa kuipatia bao la ushindi Azam dakika ya 89.
Katika mchezo huo ulioanza kwa kasi mshambuliaji Bocco alikosa bao dakika ya 33 kwa mpira wake wa kichwa kupaa juu kidogo ya lango la Vita.
Wakongo nao walijibu mapigo na kupata bao lao la kuongoza kupitia kwa Mfogang aliyetumia vizuri makosa ya beki Ibrahimu Shikanda na kupiga shuti kali akiwa nje ya 18, lililokwenda moja kwa moja wavuni.
Katika dakika ya 42 mwamuzi Dennis Batte kutoka Uganda alimuonyesha kadi ya pili ya njano Issama Mpeko, lakini akasahu kutoa kadi nyekundu na mchezaji huyo kuendelea kucheza kwa dakika kadhaa kabla ya kutolewa.
Kipindi cha pili kocha wa Azam alimtoa Jabir Aziz na kumwingiza Mrisho Ngasa, ambapo mabadiliko hayo yalikuwa na faida kubwa kwa matajiri hao wa Chamazi.
Katika dakika ya 67, mshambuliaji Bocco aliisawazishia Azam bao akiunganisha kwa kichwa krosi ya Erasto Nyoni, ambapo wakati mpira ukielekea kumalizika Ngasa alifunga bao la pili baada ya kupokea pasi nzuri ya Abubakari Salum akiwa ndani ya eneo la 18.
Kwa matokeo hayo Azam imeweka rekodi yake mpya kwa kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza na moja kwa moja imefuzu kucheza fainali.

No comments:
Post a Comment