MECHI mbili za nusu fainali ya michuano ya Kombe la Kagame, zinapigwa
leo huku mabingwa watetezi, Yanga wakikabiliwa na kibarua kigumu cha
kuwang’oa maafande wa APR ya Rwanda, mechi itakayochezwa kwenye Uwanja
wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Hiyo itakuwa nusu fainali ya pili, baada ya kuwashuhudia waalikwa AS
Vita ya DR Congo iliyowatupa nje ya michuano hiyo Atletico ya Burundi
wakikwaana dhidi ya Azam FC, inayoshiriki michuano hiyo kwa mara ya
kwanza.
Yanga chini ya Kocha Mkuu Mbelgiji Tom Sainfiet, itakutana na APR
ikiwa ni siku chache tangu wakutane kwenye mechi ya mwisho ya hatua ya
makundi na wakali hao wa Jangwani kushinda mabao 2-0.
Hata hivyo, Yanga hawapaswi kubweteka kwani timu hizo zilikutana huku
zote zikiwa na tiketi ya robo fainali, hivyo ilikuwa ni mechi ya
kukamilisha ratiba hadi Warwanda hao kupumzisha nyota wake kadhaa.
Yanga ambao msimu ujao hawatacheza michuano ya kimataifa baada ya
kumaliza msimu uliopita wakiwa nafasi ya tatu nyuma ya Simba na Azam,
watakuwa na kazi ya kupigania ushindi na hatimaye kutetea taji hilo.
Wakati Yanga wakitaka kushinda mechi ya leo na hatimaye kutwaa ubingwa
wa michuano hiyo kwa mara ya tano, APR wanataka kuubeba kwa mara ya
kwanza baada ya miaka mitano.
Yanga ikibeba taji hilo mwaka 1975, 1993, 1999 na 2011, APR wana rekodi ya kujitwisha mara mbili, 2004 na 2007.
Aidha, wakati Yanga ikitinga hatua hiyo baada ya kuwang’oa mabingwa wa
soka wa Zanzibar, Mafunzo kwa penalti 5-3, APR iliwafungasha virago URA
ya Uganda kwa mabao 2-1.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka (TFF), Boniface
Wambura, kiingilio cha kushuhudia mechi za leo kitakuwa shilingi 5,000;
7,000; 15,000 na 20,000.
Alisema, mechi ya kwanza kati ya Azam na AS Vita, itaanza majira ya
saa 8 kamili mchana kabla ya Yanga kuwakabili maafande wa APR
itakayoanza saa 10 jioni.
Akizungumza baada ya mechi ya juzi dhidi ya Simba, Ofisa Habari wa
Azam FC, Jaffar Idd Maganga, alisema kuwa kazi iliyobaki kwao ni
kuhakikisha wanashinda mechi ya leo kudhihirisha ubora wao dimbani.
Alisema ushindi wa juzi dhidi ya Simba haukuwa wa kubahatisha bali
uwezo halisi wa timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Stewart Hall na kuwasihi
wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuzidi kuipa sapoti kwa kuishangilia
No comments:
Post a Comment