
Mchezaji
wa timu ya Yanga Juma Abdul akijaribu kunyang'anya mpira kutoka kwa beki
wa timu ya Atletico Henry Mbazumutima kwenye mchezo wa pili wa fungua
dimba katika michuano ya kombe la Kagame inayoandaliwa na shirikisho la
vyama vya mpira wa miguu Afrika Mashariki CECAFA inayofanyika jijini Dar
es salaam Tanzania, Mpira umekiwasha na timu ya Yanga imeambulia kipigo
cha magoli 2-0 yaliyofungwa na mchezji Didier Kavumbagu wa Atletico

Wachezaji
wa timu za Yanga ya Tanzania na Atletico ya Burundi wakichuana vikali
katika mchezo wao uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa jioni ya leo.

Mashabiki
wa mpira wakiwa kwenye uwanja wa Taifa kwa ajili ya kushuhudia pambano
la michuano ya Kagame kwenye uwanja wa Taifa kati ya Yanga ya Tanzania
na Atletico ya Burundi

Mashabiki
wa timu ya Yanga wakiwa wamefurika uwanjani kwa ajili ya kushuhudia
mchezo kati ya timu yao na timu ya Atleticokutoka Burundi.
No comments:
Post a Comment