Wizara
ya Habari, Vijana Utamaduni, hii leo imetangaza uteuzi wa Assah
Mwambene, kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa Idara ya Habari, Maelezo.
Taarifa iliyotolewa leo hii na Wizara hiyo imesema uteuzi huo umeanza mwezi mwezi uliopita ambapo anachukua nafasi iliyokuwa imeachwa wazi na Clement Mshana ambaye mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania, TBC.
Kabla ya uteuzi huo, Mwambene alikuwa Kaimu Mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, pia aliwahi kufanya kazi katika kampuni ya magezeti ya Serikali, TSN.
taarifa via TBC, saa saba mchana.

TAMKO RASMI LA WIZARA
Bw. Asah Andrew Mwambene ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuanzia tarehe 01 Julai, 2012. Bw.
Mwambene anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Clement Mshana ambaye
mwaka jana aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji
Tanzania (TBC).
Bw. Mwambene (41) kabla ya uteuzi huu alikuwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Aidha, Bw. Mwambene amewahi kufanya kazi katika Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) akiwa mwakilishi wa Kampuni hiyo huko Zanzibar.
Idara ya Habari (MAELEZO) ndiyo Msemaji Mkuu wa Serikali hapa nchini.
IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO
AGOSTI 1, 2012

No comments:
Post a Comment