
Boris
Bunjak kocha mkuu mpya wa timu ya Azam FC akipiga picha wakati
alipotambulishwa rasmi na uongozi wa timu hiyo leo jijini Dar es
salaam, Boris Bunjak raia wa Serbia aliyezaliwa mwaka 1954 amesaini
mkataba wa kuitukimia Azam FC kwa muda wa miaka miwili akiiitumikia
timu hiyo, Boris Bunjak amefundisha timu mbalimbali katika nchi za
kiarabu na amewahi kuchezea timu ya taifa ya Serbia na vilabu
mbalimbali huko Ulaya Mashariki amewahi kufanya kazi pia katika chama
cha soka cha Yugoslavia mwaka 1993-1994 na kazi nyingine nyingi
kuhusiana na masuala ya soka.

No comments:
Post a Comment