EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, August 2, 2012

EPIQ BONGO STAR SEARCH SEARCH DAR YAVUNJA REKODI - VIJANA ZAIDI YA 5000 WAJITOKEZA SIKU YA KWANZA

Mmoja wa vijana waliojitokeza kushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search akionyesha uwezo wake wa kupiga gita lililotengenezwa kienyeji nje ya ukumbi kabla ya kukutana na majaji kwenye fukwe ya Coco jijini Dar es Salaam siku ya jana. 
Sehemu ya vijana waliojitokeza kushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search wakiwa nje ya ukumbi kabla ya kukutana na majaji kwenye fukwe ya Coco jijini Dar es Salaam siku ya jana.
Majaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search (kutoka kushoto) Salama Jabir, Ritha Paulsen na Master Jay, wakiwa "mzigoni" kwenye fukwe ya Coco jijini Dar es Salaam siku ya jana. 
Mshiriki wa BSS akijaribu bahati yake mbele ya majaji

ZAIDI ya vijana 5,000 wamejitokeza katika usaili wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba la Epiq Bongo Star Search katika fukwe za Coco siku ya jana.

Usaili huo ambao utakuwa ni wa siku tatu umeonekana kuwa ni wa aina yake hasa kutokana na idadi kubwa ya vijana waliojitokeza jana ikiwa ndio siku ya kwanza.

Katika sehemu mbalimbali za uwanja huo ilionekana kujazwa na vijana hao ambao wengi wao walikuwa wakiimba huku wengine wakiwa wanafanya mazoezi ya kutumia aina mbalimbali za vifaa vya muziki.

Akizungumzia shindano hilo, jaji mkuu wa Epiq BSS, Ritha Paulsen alisema kuwa Dar es Salaam ambao ndio mkoa wa mwisho katika usaili huo hamasa imekuwa kubwa sana kwa washiriki huku wengi wao wakiwa na matumaini makubwa ya kuchaguliwa.

"Tumeona vijana wazuri sana, na kama kawaida ya Dar tunatarajia ushindani mkali kwa mkoa huu, na ndio maana tutachukua vijana kumi na saba kutoka hapa," alisema Ritha.

Afisa Biashara wa Zantel, Sajid Khan, amepongeza umati mkubwa wa watu uliojitokeza kwa upande wa Dar es Salaam akisema kwa vipaji vilivyopatikana mwaka huu watu watarajie burudani ya kutosha vipindi vikianza kuonyeshwa kwenye luninga.

"Tunatoa zawadi kubwa kwa mwaka huu, Sh. milioni 50 pamoja na mkataba wa kurekodi, hivyo vijana wana kila sababu ya kujitokeza kwa wingi kutimiza ndoto zao," alisema Khan.

Zoezi hili litaendelea siku ya leo hii (Alhamisi) na kesho (Ijumaa) ambapo washiriki 17 watakaopatikana wataungana na wengine 33 kutoka mikoani kufikisha idadi ya washiriki hamsini watakaoingia kambini.

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate