WAREMBO wanaowania taji la Redd’s Miss Mwanza 2012, wanatarajiwa
kupanda jukwaani Ijumaa, kwenye Ukumbi wa Yacht Club, jijini hapa.
Kwa mujibu wa mratibu wa shindano hilo, Peter Omar, maandalizi yapo
sawia, hivyo akawataka watu kujitokeza kwa wingi kushuhudia fainali za
aina yake siku hiyo.
“Ninaposema kila kitu kipo vizuri, namaanisha hata kambi. Kusema
ukweli kambi ya Miss Mwanza mwaka huu ni matawi ya juu. Warembo wapo
vizuri na huduma pia ni za kiwango kizuri. Kimsingi kambi ya mwaka huu
imepandisha hadhi ya shindano letu,” alisema.
Kwa upande mwingine, Omar alisema wakongwe wa taarab nchini, Malkia
Khadija Kopa na gwiji Mwanahawa Ali, wanarajiwa kuoneshana nani mkali wa
vijembe vya mwambao kwenye shindano la Miss Mwanza 2012.
“Miss Mwanza ya mwaka huu ni funga kazi. Watakaokuja Yacht Club,
watashuhudia shoo kali ambayo haijawahi kutokea. Kwanza kabisa tuna
warembo wazuri. Hii ina maana kwamba Miss Tanzania wa mwaka huu,
atatokea Mwanza.
“Tuna timu nzuri ya wanamuziki watakaotumbuiza. Mpambano wa Khadija Kopa na Mwanahawa Ali, haujawahi kutokea Mwanza.
“Kuna wanamuziki wengine wakali watakuwepo akiwemo Bob Haisa ambaye
kwa zaidi ya miaka 14, amebaki kuwa mmoja wa mabalozi bora wa Kanda ya
Ziwa kwa upande wa muziki wa kizazi kipya,” alisema.
No comments:
Post a Comment