EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Wednesday, August 1, 2012

Kubenea, Jukwaa la Wahariri watoa tamko kuhusu MwanaHalisi kufungiwa

Picture
Saed Kubenea - Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Hali Halisi inayochapisha gazeti la Mwana Halisi akionesha baadhi ya Magazeti yaliyolalamikiwa na Serikali (picha via maasinda.blogspot.com)
WAKATI Mkurugenzi Mtendaji wa Gazeti la MwanaHalisi, Saed Kubenea akiitaka Serikali kuondoa amri ya kulifungia gazeti lake, Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limetoa tamko juu ya suala hilo.

Kubenea aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba  Sheria  ya Magazeti ya mwaka 1976 ni katili kwa sababu  haishauri Serikali kutoa maelezo ama kukumweleza mwenye gazeti juu ya nia ya kulifunga.
Kubenea alilazimika kuwaeleza waandishi juu ya suala hilo kufuatia kitendo cha Serikali  kulifungia Gazeti la MwanaHalisi kwa kile ilichodai  kuwa  mwenendo wake wa kuandika habari na makala ni wa kichochezi, uhasama na uzushi.

Alisema yeye hakuitwa kujitetea , bali alipata barua kutoka Maelezo iliyokuwa na  maelekezo ya  kwamba amezuiwa  kutoa gazeti  na kwamba asome kwenye gazeti la Serikali namba 258 la Julai 27, mwaka huu.  “Sheria hii katili ya magazeti ingali hai. Haijafutwa. Watawala wanaihitaji. Wanaitumia kutunyang’anya uhuru wa kufikiri, uhuru wa kutoa maoni na kuwasiliana, wamefanya hivyo kwa Mwanahalisi. Wametishia kufanya hivyo kwa vyombo vingine vya habari. Hii ni hatari,”alisema Mkurugenzi Mtendaji huyo.

Licha ya kuitaka Serikali kuondoa amri ya kulifungia gazeti lake, Kubenea  pia aliwaomba wasomaji wao na wadau wengine  wa habari kusimama  nao katika kudai huru na haki ya kutafuta na kusambaza habari kwa sababu nchi hii ni yetu sote.

Katika hatua nyingine, Jukwaa  la Wahariri Tanzania (TEF), limelaani kitendo cha kufungiwa kwa Gazeti la Mwanahalisi, likitoa maelezo kuwa lengo la Serikali ni kuviziba midomo vyombo vya habari ili visifichue uovu unaofanywa katika mfumo wa utawala.

Taarifa ya jukwaa hilo ilisema kuwa,  sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo Serikali imeitumia kulifungia gazeti hilo,  ni moja ya sheria ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na kuwa mara kadhaa yamekuwapo mapendekezo kwamba sheria hizo zifutwe.

“Uamuzi wa kulifungia MwanaHalisi haukubaliki na tunauona kama mwendelezo wa jitihada za Serikali kukandamiza uhuru wa habari na wanahabari nchini, lengo likiwa ni kuwaziba midomo wasiseme ukweli kuhusu uovu unaofanyika katika mfumo wetu wa utawala na jamii kwa ujumla,” ilisema sehemu ya taaifa ya TEF iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Neville Meena.

Ilisema pia kuwa,  uamuzi huu wa Serikali unaonekana una nia mbaya ndani yake, kwani adhabu ya kulifungia kwa muda usiojulikana ina tafsiri pana kwani inawezekana lengo la Serikali ni kulifuta gazeti la MwanaHalisi kijanja.

Naye wakili wa gazeti hilo, Legemeleza Nshala  alisema  Serikali  ilikiuka ibara ya 18 kifungu cha 26 (1) na cha (2) na kifungu cha 30 (1) na cha 8 (2) (a)-(e) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977.  Alisema pia kuwa imekiuka Ibara ya 19 ya Agano la Kimataifa  la Haki  za Binadamu la mwaka 1966 na Ibara ya 6 ya Agano la Fungamano la Afrika Mashariki pamoja na Ibara ya 8 ya Agano la Haki za Binadamu  na watu la Afrika la mwaka 1981.
Fredy Azzah na Tausi Ally 
MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate