MWAKILISHI wa Tanzania katika Miss World, Lisa Jensen ameanza vizuri
katika mashindano hayo baada ya kufanikiwa kuingia kumi bora ya shindano
la Top Model, hivyo amepata pointi zaidi kabla ya fainali za mashindano
yenyewe kufanyika.
Lisa Jensen
Lisa Jensen
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Mongolia ambapo
shindano la Miss World litafanyika, Lisa alianza vizuri kwa sababu ya
uwezo wake mkubwa, huku akionesha kipaji cha aina yake katika shindano
hilo lililofanyika juzi usiku nchini humo.
Akithibitisha habari hizo, Ofisa Habari wa Kamati ya Miss Tanzania , Haidan Ricco alisema Lisa ni mmoja kati ya wawakilishi watatu kutoka Bara la Afrika ambao wamefanikiwa kupenya na kuingia katika nafasi hiyomuhimu.Waafrika wengine waliofanikiwa kupenya katika kumi bora ya shindano hilo kabla ya siku ya fainali ya Miss World ni mrembo wa Afrika Kusini na Shelisheli.
Hata hivyo baada ya Lisa kuingia kumi bora, bado ana kazi kubwa ya kuhakikisha anapambana ndani ya wiki hii wakati mshindi wa Top Model atakaposakwa rasmi.
“Kwetu sisi ni faraja kubwa mno, kwani tunaamini Lisa ataiwakilisha vema Tanzania na huu ni mwanzo mzuri kwake,” alisema Ricco, huku akiwataka Watanzania wamuombee kabla ya kufanyika shindano la Miss World hapo Agosti 18.
Shindano la Miss Tanzania kwa sasa linadhaminiwa na kinywaji cha Redd’s, ambacho kinazalishwa na Kampuni ya Bia Tanzania .

No comments:
Post a Comment