Mwanamke mkazi wa kijiji cha Isima
Wilaya ya Geita, Monica Mapori (22), amejinyonga kwa kutumia kipande cha
kitenge chake eneo la Hospitali ya Wilaya ya Geita muda mfupi baada ya
mtoto wake kufariki dunia.
Mtoto huyo alikuwa amelazwa hospitalini hapo kwa matibabu.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dk. Nelson Bukulu, alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo.
Dk. Bukulu, alimtaja mtoto aliyeaga dunia kuwa ni Tumaini Philemon, mwenye umri wa miezi 18 na kwamba alilazwa hospitalini hapo kutokana na maradhi ya pumu.
Alifafanua kuwa mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa unaning'inia ndani ya eneo la uzio wa hospitali hiyo.
"Baada ya uchunguzi wa polisi na madaktari, utakabidhiwa kwa ndugu zake kwa mazishi," alisema.
Mume wa marehemu, Philemon Kabulaya (24), alisema kwa simanzi kuwa huenda mkewe alifikia uamuzi huo kutokana na kifo cha mtoto wao mpendwa.
Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Paulo Leonard, alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo.

No comments:
Post a Comment