EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Thursday, August 2, 2012

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi jijini Dar es Salaam, imesema mgomo wa walimu ni batili imeitaka CWT kuwatangazia Walimu warudi Kazini

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi jijini Dar es Salaam, imesema mgomo wa walimu ni batili kwasababu haukuzingatia matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazi ya mwaka 2004 na uliandaliwa kwa dhamila mbaya.

Jaji Sophia Wambura wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo jana saa 9:14-37 alasiri huku ukumbi wa wazi wa mahakama hiyo ukiwa umefurika walimu ambapo katika uamuzi wake huo pia aliwataka walimu wote kurejea mara moja kazini.

Jaji Wambura alisema asikiliza kwa makini hoja za mawakili waandamizi wa serikali Pius Mboya na Obadia Kameya ambao walikuwa wakiwawakilisha walalamikaji katika maombi hayo madogo namba 96/2012 yaliyoletwa chini ya hati ya dharula na Katibu Mkuu Kiongozi, Katibu Mkuu Ofisi ya rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Mwanasheria Mkuu wa Serikali na ya mdaiwa ambaye ni Chama cha Walimu Tanzania (CWT) ambao walikuwa wakiwakilishwa na wakili wa kujitegemea Gabriel Mnyele.

Jaji Wambura alisema mgogoro uliowasilishwa mbele yake na walalamikaji ni kwamba wanaiomba mahakama hiyo itamke kuwa mgomo wa walimu ni batili wakati wakili wa CWT, Mnyere alidai mgomo huo ni halali kwa sababu umekidhi matakwa ya sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini.

Jaji huyo alisema mahakama yake imefikia uamuzi wa kutofautiana na zoezi la upigaji kura za kuunga mkono mgomo ambalo liliendeshwa na CWT ambapo asilimia 97 ya walimu waliinga mkono kuanza kwa mgomo kwasababu zifuatazo:

  • “Mosi, zoezi lile la upigaji kula lilikuwa likiwadanganya wanachama wa CWT kuwa zoezi hilo limeendeshwa rasmi na kwa mujibu wa sheria, zoezi lile halikukidhi matakwa ya sheria kwa sababu wanachama wake walikuwa hawajaelewa na viongozi wa chama hicho madhara ya kufanya mgomo huo, zoezi lile halikufuata taratibu; 
  • Notisi ya kugoma iliyotolewa na CWT Julai 27 mwaka huu saa tisa alasiri wakati zoezi la upigaji kura zile lilikuwa bado halijafanyika na kwa sababu hiyo zoezi lile likikuwa batili;
  • Kwa mdaiwa (CWT) kushindwa kufuata matakwa ya kifungu cha 42 na 43 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini,ni wazi taratibu zote walizozifanya za kupiga kura ya kuunga mkono mgomo na kugoma mdaiwa alizifanya akiwa na dhamila mbaya kwani wajumbe wa chama hicho hakuwa na makubaliano ya jinsi mgomo utakavyoendeshwa na kusimamiwa,” alisema Jaji Wambura huku baadhi ya walimu wakiwa wamejiinamia.”  

Alisisitiza kuwa, CWT imeitisha mgomo huo ikiwa na dhamira mbaya kwasababu ni CWT ndiyo alikataa kuendelea na mazungumzo na mwajiri wake badala yake akaanzisha mgomo wakati Julai 27 mwaka huu, pande zote katika hizo zilifika mbele yake kuomba na upande wa mlalamikaji ukaomba mahakama itoe amri ya kutaka pande zote zisiendelee na jambo lolote hadi mahakama itakapowasilikiliza lakini cha kushangaza siku hiyo hiyo saa tisa alasiri CWT ilienda kutoa noti ya kuanza mgomo kwa walimu nchi nzima ndani ya saa 48 wakati kulikuwa na amri ya mahakama iliyozitaka pande zote kutoendelea kufanya jambo lolote linalohusiana na kesi hiyo ambapo mgomo huo batili ulianza rasmi nchi nzima kuanzia Jumatatu ya wiki hii na hadi sasa unaendelea.

“Kwa maelezo hayo hapo juu nasisitiza mgomo huo ni batili kwani haujakidhi matakwa ya kifungu cha 84(1),(2) cha Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya mwaka, na mgomo uliondeshwa kwa siku tatu sasa ni batili na ninaamuru mgomo huo usitishwe mara moja na walimu wote warejee kazini na kwa kuwa mdaiwa aliitisha mgomo huo kwa mkutumia taarifa kwa vyombo vya habari pia naamuru kiongozi aliyetoa taarifa hiyo ya mgomo aende tena kwenye vyombo vya habari akatangaze kuwa mgomo waliokuwa wakiufanya ni batili na kuwataka walimu warejee kazini mara moja na mahakama hii imemshangaa sana wakili Mnyere kwa kushindwa kuwashauri wateja wake mapema kwamba mgomo waliokuwa wakiundesha ulikuwa umekiuka sheria,”

alisema Jaji Wambura na kuongeza;

“Aidha, naiamuru CWT kulipa gharama na fidia kwa kipindi chote ambacho wanafunzi wamekosa vipindi kwaajili ya mgomo huo batili na kama pande zote zinaona kuna hata ya kurudi meza ya majadiliano zilirudi kwenye meza ya majadiliano na zimualike mtaalamu wa sheria za kazi awasaidie kufikia mwafaka.”

Baada ya hukumu kutolewa, baadhi ya viongozi wa CWT waliwaomba waandishi wa habari waje nje ya mahakama kwani kutakuwa na mkutano lakini hata hivyo waandishi walipofika nje ya viwanja hivyo mahakama walimkuta Rais wa chama cha walimu, Gratian Mkoba akiwa amenyongonyea na hata alipotakiwa atoe tamko ni lini atatekeleza amri ya mahakama iliyomtaka aende kwenye vyombo vya habari autangazie umma kuwa mgomo alioutisha ni batili na awatake walimu warudi kazini alishia kusema leo atafanya mkutano na waandishi wa habari na kwa upande wa wakili wao Mnyere alisema amekubaliana na uamuzi huo wa mahakama.
via HappyKatabazi.blogspot.com

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate