SERIKALI
itakuwa inagawa ng’ombe 1500 kila mwezi kwa wananchi wa wilaya tatu za
Mkoa wa Arusha kama kifuta jasho cha kupoteza kiasi cha karibu mifugo
800,000 iliyopotea kutokana na ukame na athari zake mwaka 2008/2009.
Ahadi
hiyo imetolewa leo, Alhamisi, Agosti 2, 2012 na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wakati
alipozindua Mradi wa Serikali wa Uwezeshaji Mifugo kwa waliopotelewa
mifugo yote katika Wilaya ya Monduli kwenye sherehe iliyofanyika
Makuyuni wilayani humo.
Katika
uzinduzi huo uliohudhuriwa na viongozi wa Mkoa wa Arusha wakiwemo wakuu
wa wilaya na wabunge wa mkoa huo, Rais Kikwete amegawa ng’ombe 500 kwa
kundi la kwanza la wananchi ikiwa ni mitamba minne na dume moja la
kisasa kwa kaya 16 za mwanzo.
Uzinduzi
huo ni wa pili kufanywa na Rais Kikwete chini ya Mradi huo wa kwanza wa
aina yake kubuniwa na Serikali katika historia na wenye thamani ya sh.
Bilioni 12.9.
Februari
19, mwaka huu, Rais Kikwete alizindua Mradi kama huo katika Wilaya ya
Loliondo kwenye sherehe zilizofanyika mjini Loliondo. Kesho Agosti 3,
2012 Rais Kikwete anatarajiwa kuendelea na zoezi hilo katika mji wa
Loliondo
No comments:
Post a Comment