EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Saturday, August 25, 2012

Mfanyakazi wa nyumbani Kigamboni auawa na mfanyakazi mwenzie na kuzikwa

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam linamshikilia kijana Yuda Paul (30), mkazi wa Kisiwani Kigamboni, kwa tuhuma za mauaji ya mfanyakazi wa ndani, Flora Tadei, ambaye alimzika katika uwanja wa tajiri yao.

Akizungumza na gazeti la NIPASHE jijini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Agosti 23 mwaka jana akiwa nyumbani kwa tajiri yake huko Kigamboni.

Kamanda alisema Flora alikuwa ni mfanyakazi wa ndani katika eneo hilo na pia ni mkazi wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara na mtuhumiwa huyo alikuwa ni mfanyakazi bustani katika nyumba hiyo.

Alisema wakiwa wanafanya kazi kwa pamoja, siku ya tukio mtuhumiwa na marehemu waliachwa nyumbani na bosi wao aliyekuwa ameenda kazini ambapo Paul alimuua marehemu huyo na kumzika kwenye uwanja wa tajiri yao. Baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alichukua baadhi ya vitu vya ndani ya nyumba na kwenda kuvitupa porini ili kujenga mazingira ya kuonyesha kuwa marehemu alimuibia tajiri huyo na kutoroka.

Alisema mke wa bosi wao aliporejea kutoka kazini aliamini kuwa ni kweli marehemu huyo amemuibia na kuamua kwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Kigamboni.

Tangu kipindi hicho mpaka sasa waliamini kuwa marehemu amewaibia na anatafutwa na polisi huku ndugu wa marehemu wakijua kuwa ndugu yao ni mzima na anafanya kazi Kigamboni.

Kamanda Misime alisema polisi inaendelea na uchunguzi wake ikiwa ni pamoja na kuufufua mwili wa marehemu huyo ambao umekutwa umeshaoza na kubakia mifupa. Alisema mwili wa marehemu huyo umehifadhiwa kwa ajili ya kusubiriwa ndugu zake kwa ajili ya mazishi. Kamanda alisema ndugu wa marehemu huyo bado hawajapatiwa taarifa juu ya kifo hicho kwani wanajua ndugu yao anaendelea na kazi.

Alisema uchunguzi dhidi ya tukio hilo utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani.

via gazeti la NIPASHE

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate