LE meli maarufu kwa jina la ‘Meli ya Magufuli’ ambayo serikali
iliinasa katika eneo lake la bahari ya Hindi ikivua samaki bila ya
kibali, imezama baharini.
Meli hiyo ambayo ina uwezo wa kuvua samaki kwenye kina kirefu baharini, imezama baada ya wajanja wachache kukata vyuma vyake na kuuza kama chuma chakavu.
Kwa mujibu wa habari hizo, wajanja wamekuwa wakiingia na kukata vyuma
vya meli hiyo baada ya serikali kuitelekeza kwa muda mrefu bila
uangalizi tangu ilipoitaifisha.
Vyanzo vyetu vya habari vilipasha kuwa vyuma chakavu vya meli hiyo vimekuwa vikiuzwa kwa kampuni zinazonunua na kuvisafirisha nje ya nchi na kujiingizia mabilioni ya fedha.
Sehemu kubwa ya vyuma chakavu kutoka kwenye meli hiyo, vimeuzwa kwa
kampuni moja inayomilikiwa na mmoja wa wabunge wa Jamhuri ya Muungano.
Inaelezwa kuwa sehemu kubwa ya meli hiyo imetengenezwa kwa malighafi aina ya Brass ambayo kilo moja kwa sasa inauzwa kwa sh 5,200.
Malighafi nyingine zilizotumika na bei yake kwa kilo kwenye mabano
vikuzwa kama chuma chakavu ni Cast Aluminum (sh 1,700), Stainless (sh
1,500) na Soft (sh 2,000).
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mathayo David Mathayo alipotafutwa kwa
njia ya simu kuzungumzia meli hiyo, alisema yuko mkutanoni na kutaka
atafutwe baadaye kutolea ufafanuzi.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Waziri Mathayo alikiri kuwa kweli meli hiyo imezama na amepata taarifa hizo.
“Ni kweli imezama na sisi tumepata taarifa hizo, lakini kama wizara
tulikuwa hatujakabidhiwa meli hiyo kwani ilikuwa kielelezo cha polisi
wakati kesi ilipokuwa mahakamani na haijawahi kukabidhiwa kwetu,”
alisema Waziri Mathayo.
Meli hiyo, Tawaliq 1, ilikamatwa Machi 8, 2009 ikiwa na tani 293 za
samaki aina ya Jodari iliyowavua katika bahari ya Hindi ndani ya Ukanda
wa Kiuchumi wa Tanzania (EPZ) bila kibali.
Ilikamatwa ikiwa na wavuvi 34 na hadi kufikia tamati ya kesi hiyo, 20 walitiwa hatiani.
Lakini licha ya mahakama kuamuru meli hiyo itaifishwe kwa sababu
ilikuwa haijulikani na tume inayojihusisha na shughuli za uvuvi katika
Bahari ya India (IOCT) ilitelekezwa.
Kwa mujibu wa habari hizo, meli hiyo ilianza kuzama tangu mwaka jana huku wizara husika ikiangalia bila kuchukua hatua.
Meli hiyo ilikamatwa na Waziri Dk. John Magufuli mwaka 2009 wakati huo akiwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi.
Via Tanzania Daima
No comments:
Post a Comment