Akataa kuomba radhi, asema tuhuma atazithibitisha mahakamani, Amtaka
Dk. Slaa kuandaa bilioni 3 na shilingi moja. Ni kwa kudai CCM inaingiza
silaha nchini.
KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye
amewataka Chadema kwenda mahakamani haraka badala ya kusubiri kuombwa
radhi kama walivyotaka ili kusafishwa dhidi ya madai ya chama chao
kupewa mabilioni ya fedha na mataifa tajiri.
Aidha amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dk. Wilbrod Slaa kuiomba
radhi CCM la sivyo itamburuza mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3 na
shilingi moja, kwa kuituhumu uongo kwamba imeingiza silaha kutoka nje
ya nchi tena bila kulipia ushuru.
Nape alisema hayo leo Agosti 27, 2012, kwenye mkutano wake na
waandishi wa habari, uliofanyika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa
wa Lumumba mjini Dar es Salaam.
“Bila shaka mmesikia jana Chadema wakinitaka niombe radhi au
wananipeleka mahakamani kudai fidia ya sh. bilioni 3, kwa madai eti
nimesema Chama hicho kinapata mabilioni ya fedha kutoka kwa mataifa
tajiri. Mkubwa hatishiwi nyau, nawataka waende haraka mahakamani wala
wasisubiri hizo siku saba”, alisema Nape.
Alisema, CCM inao ushahidi wa kutosha kuhusu madai aliyotoa Nape
dhidi ya Chadema na kwamba huyo tayari kutoa uthibitisho huo mahakamani
badala ya kuomba radhi.
“Nadhani wakienda mahakani itapendeza zaidi maana huko ndiko pazuri
kutoa uthibitisho kuhusu tuliyosema, na ninawahakikishieni
tukishathibitisha na Msajili wa Vyama akaupata uthibitisho huo chama
chao kinafutwa”, alisema.
Kuhusu CCM kumburuza Dk. Slaa mahakamani, Nape alisema, ameshawaagiza
wanasheria wa Chama, kuandaa barua ya kusudio la mashitaka hayo, na Dk.
Slaa atapelekewa ili aamue kama ataomba radhi au atakuwa tayari kwenda
mahakamani.
“Wakati wanakwenda mahakamani, Chadema wamwambie babu yao ajiandae
kuomba radhi au kuburuzwa mahakamani kuilipa CCM fidia ya sh. bilioni 3
na shilingi moja kwa kuizushia CCM uongo kwamba inaingiza silaha nchini
tena”, alisema Nape.
Bashir Nkoromo
Blogger & Senior Photojournalist
Uhuru Publications Ltd,
Publishers of Uhuru, Mzalendo and Burudani tabloids
Cell; +255 712 498008, +255 789 498008, +255 773 600007 +255 756 646131
E-mail: nkoromo@gmail.com, bnkoromo@yahoo.com.
P O Box 9221, Dar es Salaam.Tanzania, East Africa
Blogger & Senior Photojournalist
Uhuru Publications Ltd,
Publishers of Uhuru, Mzalendo and Burudani tabloids
Cell; +255 712 498008, +255 789 498008, +255 773 600007 +255 756 646131
E-mail: nkoromo@gmail.com, bnkoromo@yahoo.com.
P O Box 9221, Dar es Salaam.Tanzania, East Africa
No comments:
Post a Comment