Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Street Children Sports Academy TSC
ya Mwanza Bw. Mutani Yangwe akizungumza na waandishi wa habari leo
katika ofisi za Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF Karume wakati
akielezea mafanikio ya timu ya Academy yao waliyoyapata kutoka nchini
Ujerumani na kunyakua mataji mbalimbali na zawadi kemkem. amesema
takribani wachezaji saba wamefanikiwa kupata ofa ya kufanya majairibio
nje watatu wakihitajika katika timu ya Makabi Haifa ya Israel na
wengine wanne wakipata ofa kwenda nchini Sweden ambako watapitia kisha
kwenda nchini Ujerumani. Katikati katika picha ni Altaf Hirani Rais wa
kituo hicho na kushoto ni kocha wa kutuo hicho Bw. Rogashian Kaijage
Altaf Hirani Rais wa Taasisi ya Tanzania Street Children Sports
Academy TSC ya Mwanza akizungumza na waandishi wa habari leo kwenye
ofisi za shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania TFF kulia ni
Mkurugenzi wa TCS Mutani Yangwe na kushoto ni Mmoja wa maofisa wa kituo
hicho B. Leonard Magomba.
Viongozi
wa kituo hicho wakiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu hiyo
kutoka TCS Mwanza mara baada ya kuzungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es salaam wakiwa na mataji yao waliyoijishindia na zawadi
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment