AFRIKA imefanikiwa kuvusha warembo sita kati ya 47, kuchuana katika
hatua ya nusu fainali katika shindano dogo la Miss World linalojulikana
kama 'Top Model'.
Katika warembo hao, yumo mrembo kutoka taifa jipya lililojipatia uhuru wake miezi michache iliyopita, Sudan ya Kusini iliyojitenga na Khartoum.
Mrembo wa Tanzania Lisa Jensen, aliishia hatua ya robo fainali ya shindano hilo, ambapo warembo waliokata tiketi watachuana kuwania nafasi 15 kwenda fainali.
Fainali ya shindano hilo la Top Model, ambalo ni miongoni mwa mashindano madogo saba ya Miss World litafanyika Agosti 12.
Mataji mengine madogo ya Miss World ni pamoja na Mrembo Bora wa Ufukweni, Michezo, Urembo kwa Malengo, Multmedia, Ubunifu wa Mitindo.
Walimbwende wa Afrika walioingia hatua hiyo ni, Atong Demach kutoka Sudan Kusini, Damiete Charles-Granville (Nigeria) na Shamim Nabil (Kenya).
Wengine, Edmilza dos Santos (Angola), Marie-Noelle Ada (Gabon) na HÈlËne-Valerie Djouka (Ivory Coast).
Shindano kamili la Miss World ambalo kwa mwaka huu litakuwa likifanyika kwa mara ya 62 tangu mwaka 1950, litafanyika, China Agosti 18 na kuwashirikisha warembo 116.

No comments:
Post a Comment