HALMASHAURI ya Wilaya ya Sengerema kwa kushirikiana na wafadhili kutoka
Korea Kusini wanatarajia kujenga hospitali ya meli kwa ajili ya kutoa
matibabu kwa wananchi wanaoishi katika visiwa vilivyopo katika ziwa
Victoria.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, Mathew Lubongeja amelieleza gazeti la MTANZANIAa kuwa meli hiyo itajengwa maalumu kwa ajili ya kutumika kama hospitali inayotembea.
Lubongeja alisema tayari vifaa vya kujenga meli hiyo vimekwisha kuwasili katika bandari ya Dar es Salaam kutoka Korea Kusini na vinatarajiwa kusafirishwa wakati wowote kupelekwa Mwanza kwa ajili ya kuunganishwa na kuwa meli kamili.
Alisema hospitali hiyo inayotembea itakuwa ikitoa huduma za matibabu kwa wananchi wanaoishi katika visiwa na itakuwa na uwezo wa kulaza wagonjwa na kutoa huduma zote muhimu ikiwa ni pamoja na upasuaji.
"Meli hiyo ni ya aina yake, wananchi wanaoishi katika visiwa katika ziwa Victoria walikuwa na tatizo la kupata huduma ya hospitali kutokana na mazingira yao, tumejitahidi kutafuta wafadhili na ndoto yetu imetimia wananchi hao watapata hospitali ya uhakika inayotembea," alisema.
Lubongeja alisema kazi ya kuiunganisha meli hiyo itakayotumika kama hospitali inatarajiwa kuchukua muda mfupi na kuwapongeza wafadhili hao kwa msaada huo.
Wilaya ya Sengerema inaongoza kwa kuwa na visiwa vingi katika ziwa Victoria. kwa kuwa na visiwa 37 hali ambayo imekuwa ikisababisha wananchi wengi kukosa huduma za matibabu kutokana na kutokuwapo usafiri wa uhakika.
via MTANZANIA

No comments:
Post a Comment