EFM RADIO

EFM RADIO

HERICONY

Tangaza hapa

Tangaza hapa

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

TANGAZA NA BLOG YAKO HAPA

Sunday, September 9, 2012

Baba yake Dk Ulimboka atoa ya moyoni


BAADA ya kimya cha muda mrefu, baba mzazi wa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk Stephen Ulimboka, amekubali kuzungumzia sakata la mwanaye kutekwa, kuteswa, kutibiwa na hatimaye kurejea nchini akisema kwamba kupona kwake ni neema za Mungu, huku akiishutumu Serikali kuwa imewatelekeza Watanzania.
Hii ni mara ya kwanza kwa baba huyo, Ulimboka Mwaitenda kuzungumza tangu mwanaye alipotekwa, kuteswa na baadaye kutupwa katika Msitu wa Pande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

“Naishangaa Serikali hii ambayo wananchi wanapigwa na kuuawa bila makosa. Nakumbuka kiongozi aliyeipenda Tanzania ni mmoja na ameshatangulia mbele za haki,” alisema akimaanisha Baba wa taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Mwaitenda alitoa kauli hiyo jana baada gazeti hili kumtafuta ili azungumzie habari zilizoenea nchini kwamba mwanaye, amepata kazi nje ya nchi.

Kuhusu madai hayo, Mwaitenda alikanusha akisema kuwa mtoto wake hawezi kwenda nje ya nchi bila yeye kufahamu... “Pengine ana mipango hiyo, lakini mimi sijui wala sijasikia, lakini atakwenda nje ya nchi kufanya nini? Hizi habari hizo ndiyo nazisikia kwako kwa mara ya kwanza eti Ulimboka anataka kwenda nje ya nchi? Akafanye nini alichokosa hapa Tanzania!”

Wakati mwandishi akiingia nyumbani kwa Mwaitenda, Ubungo Kibangu, Dar es Salaam, alipishana na Dk Ulimboka akiwa kwenye gari na wenzake, wanne. Hata hivyo, hakufanikiwa kuzungumza naye.
Kuhusu tukio la kutekwa, kuteswa na kutupwa katika Msitu wa Pande, Mwaitenda alisema: “Mpaka sasa, tumeiona kazi ya Mungu, ile ni neema ya Mungu kwa sababu wewe uliona wapi mtu akapigwa namna ile halafu akapona kama si kwa neema tu.”
Alisema alimkanya mtoto wake huyo aachane na masuala ya migomo na siku chache baada ya onyo lake ndipo akatekwa na kujeruhiwa vibaya.

“Nilimkanya kabisa kuhusu mambo ya migomo hasa baada ya kuniambia kuwa amechaguliwa kuwa msemaji mkuu wa madaktari wenzake na kwa bahati mbaya ndiyo yakatokea hayo yaliyotokea,” alisema.
Alielezea kushangazwa kwake na watu waliompiga mtoto wake akisema, hajui walikuwa wanataka nini. Alisema hakuwa na uhasama na mtu yeyote kuanzia kazini kwake hata kwa marafiki zake.
“Mpaka sasa nashindwa kuelewa kwa nini waliamua kumpiga, kwa sababu kwa ninavyomjua Steven, hajawahi kuwa na ugomvi na mtu tangu anasoma shule ya msingi mpaka anamaliza chuo kikuu. Sijawahi kupata mashtaka kuwa amegombana na mtu. Nashangaa haya yanayotokea leo.”
Akitoa wasifu wa mwanaye huyo alisema tangu utoto wake, daktari huyo alikuwa mtulivu na mwenye upeo wa hali ya juu. Alisema anasikitishwa mno na yaliyompata akisema kwamba siku moja ukweli utawekwa wazi  kwani siku zote kazi za Mungu na kazi za shetani haziwezi kuchangamana.

“Kama mafuta na maji, ukiyachanganya... mafuta yatakuwa juu na maji yatabaki chini. Najua siku moja Mungu ataweka wazi ukweli,” alisema.

Kuhusu afya ya Dk Ulimboka, Mwaitenda alisema ingawa yeye si daktari, lakini anamwona mtoto wake kuwa yu mwenye afya na kuongeza kuwa hata mwanaye huyo amekuwa akisema kwamba sasa ana afya njema.

Hali nyumbani kwa Mwaitenda
Baada ya kufika nyumbani kwa mzazi huyo wa Dk Ulimboka, mwandishi alikaribishwa vyema na mzazi huyo ingawa alimtahadharisha kwamba endapo angekutana na daktari huyo hapo au ndugu zake, wangemfukuza.

“Una bahati ungewakuta hapa watoto wangu tusingezungumza. Hata hawa mabinti zangu wakikukuta, hatutaendelea na mazungumzo....”
Hivyo ndivyo ilivyotokea kwani baada ya kuelezea hayo, mabinti wake wawili walitokea na mmoja akaanza kwa kusema... “Shikamoo Baba, umesharudi? Huyu nani?”
Mzee Mwaitenda, kwa bashasha aliwatambulisha mabinti hao... “ Huyu ni Florence... mwandishi wa Mwananchi...” Hata kabla hajaendelea binti huyo na mwenzake walimshika mkono na kumwamuru atoke nyumbani hapo mara moja.

“Haya dada toka, toka, mmeshindwa kuandika kuhusu mwandishi mwenzenu aliyekufa (Daudi Mwangosi), mnakuja kutufuata mpaka huku Kibangu.... mtazame miguu ilivyomchafuka kwa vumbi kwa kushadadia ya watu, toka kabla sijakupiga makofi,” alisema mmoja wa mabinti hao.

Madai Dk Ulimboka kutoweka
Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk Namala Mkopi ambaye alikuwa karibu na Dk Ulimboka wakati wa mgomo wa madaktari nchini, alisema tangu waonane aliporejea nchini kutoka Afrika Kusini, hajawasiliana tena.

“Hatujawasiliana naye,” alisema Dk Mkopi na kusema kulingana na ukubwa wa tatizo lililompata, hakuwa na mpango wa kumsumbua, bali kumwacha apumzike hadi atakapokuwa amejisikia mwenyewe kurejea kazini.
Aliyekuwa kiongozi wa jopo la madaktari waliomhudumia, Profesa Joseph Kahamba alisema, hajawahi kuonana wala kuwasiliana na Dk Ulimboka tangu alipopelekwa Afrika Kusini, Juni mwaka huu.

CHANZO >>> www.mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment

HABARI MBALIMBALI

‘Dk. Cheni’ ‘Sharo Milionea ‘Thea’ African Women AGNESS MASOGANGE AK CLASSIC COSMETICS ALI KIBA Amanda Poshy Ant ANT LULU Ashley Toto Aunt Ezekiel Aunty Ezekiel AUNTY LULU Azam Fc Baby Madaha BAHATI BUKUKU Barnaba BATULI BBA Beauty of the day Belle 9 BI KIDUDE BIBI BOMBA Big Brother Big Brother Africa Bill Gates BINTI KIZIWI BOB JUNIOR Bodi ya Filamu Bongo Movie Bongo Movies CCM CHADEMA Chombezo Christina Shusho Chuchu hans. Clouds Media Group Club Bilicanas DAR LIVE DAVINA Dayna Nyange Diamond Dida Diva Loveness Love Dj Ommy Crazy wa Maisha Club DOGO JANJA DOKI DR.CHENI DSTV Dude Dully Sykes EBSS 2013 Elizabeth Michael Epiq Bongo Star Search (EBSS) ESHA BUHETI Ester Bulaya Feza Kessy FIESTA 2014 Flaviana Matata FLORA MBASHA FLORA MVUNGI Francis Cheka GARDNER GLOAL PUBLISHERS GLOBAL TV ONLINE H. BABA Halima Mdee HAMISA Happy birthday Hemedi Hemedy Suleiman HOTUBA YA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Hoyce Temu Huddah Monroe HUSINA IRENE PAUL Irene Uyoya ISABELLA J film 4 life Jack Chuz JACK PATRICK Jacob Steven ‘JB’ Jacqueline Dustan JACQUELINE WOLPER Jaji Khamis 'Kashi' Jay Dee JENNIFER KYAKA (ODAMA) JIDE JINI KABULA JK JO Johari Jokate Mwigelo ‘Kidot’. JOTI Joyce Kiria Joyce Kiwia JUX K-LYNN KADINDA kaja Kajala Masanja Kapotive Star Singers KATUNI Kemmy Kero Zetu KHADIJA OMAR KOPA KIKWETUKWETU KILI MUSIC AWARDS KOLETA Lady Jay Dee Lady Jaydee Lake Oil LAVEDA Linah Sanga Linex Lisa Jensen Loveness Diva Lucy Francis Komba Lulu M2 The P MABILIONEA Madam Rita MADELA Magazeti Mahusiano Maimartha Jesse MAINDA MAISHA Makala Malkia Elizabeth MAMTEI MANDELA MARIAM ISMAIL Masanja Mkandamizaji Mashindano ya Miss Tanzania Matangazo Matonya MaxMalipo MAYA MELLIS EDWARD MENINAH MGOSI MKOLONI Mh Halima Mdee mic Michezo MILLEN HAPPINESS MAGESE MISS CHANG'OMBE MISS DAR CITY CENTER Miss East Africa MISS REDD'S IRINGA 2013 MISS TANGA 2013. MISS TANZANIA 2014 Miss Tanzania mwaka 2011 MISS TEMEKE 2014 MISS USTAWI MISS UTALII TANZANIA 2012/13 Miss vyuo vikuu 2013 MKALA MREMBO HUDDAH Mrisho Mpoto Mrisho Ngassa MSHINDI WA REDD'S MISS LAKE ZONE 2013 NI LUCY CHARLES. MSHINDI WA TAJI LA REDDS MISS KANDA YA KATI 2013 Mtitu muziki Mwana FA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Mzee Majuto Nancy Sumari Nani Mtani Jembe? NAPE Nassoro ‘Nora’ Natasha Nay wa Mitego Necta Nelly Kamwelu NEY WA MITEGO Nisha NSSF;Zantel Nyamwela NYimbo Nyota yako OBAMA TANZANIA OMMY DIMPOZ P FUNK PAM D Peniel Mgilwa ‘Penny’ PETIT MAN Profesa Jay Q - CHILA Q Boy Q Chilla QUEEN DARLEEN RACHEL NDAUKA RAIS KIKWETE Rais Kikwete. Rasimu Ya Katiba TZ Ray Ray C Redd’s Miss IFM REDD'S MISS KAGERA 2013 REDD'S MISS TZ REDDS MISS TANZANIA 2014 Redds Miss wa Mikoa REHEMA FABIAN RICHIE RICHIE Rihanna ROSE MUHANDO Rose Ndauka Ruge Mutahaba. SABASABA 2013 Saida Karoli Saikolojia Sajeti SAJUKI Sandra SHAA Shamsa Ford Sheikh Ponda Shilole Sintah Siwema Skin Tricks Snura Mushi Spika Makinda staa Staa Wetu Stella Mwangi STYLE ZA NYWELE Taifa Stars Tamasha la matumaini TAMASHA LA SERENGETI FIESTA 2013 Tangazo TANZANIA TEGO TENGENEZA WEBSITE NA BLOG TID Tundaman Tupo wangapi? TUZO ZA MWANAMKE BORA WA MWAKA 2013/14 Twanga Pepeta USA PAGEANT 2014‏ VAI Wastara WEMA WEMA SEPETU Yanga Yanga Bingwa 2013 YOUNG D Yvonne Cherry ‘Monalisa’ Z Anton. Zari Zito kabwe

Translate