Mwakilishi wa Radio One wilayani Masasi, Rashid Kanga amefariki dunia jana katika Hospitali ya Mkomaindo iliyopo Wilayani humo, alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Alifariki jana asubuhi kwa kusumbuliwa na Malaria na upungufu wa damu na alizikwa siku hiyo hiyo katika makaburi ya Mjini Masasi Mkoani Mtwara.
Akielezea kifo hicho Mwandishi wa Habari wa Kituo cha Televisheni cha Chanel Ten, mkoani Mtwara John Kasembe, alisema wamehuzunishwa na kifo cha mwenzao ambaye alikuwa ni mmoja wa wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoani humo.Kasembe alisema kutokana na uzoefu wa muda mrefu katika fani yake ya habari, marehemu alikuwa mshauri wa wanahabari mkoani humo.
No comments:
Post a Comment